UGIRIKI-WAKIMBIZI

Ugiriki mbioni kuiacha tupu kambi ya Idomeni

Katika kambi ya wakimbizi ya Idomeni katika mpaka kati ya Ugiriki na Makedonia, wakimbizi wakiusubiri kuendelea na safari yao hadi kaskazini (Machi 17, 2016).
Katika kambi ya wakimbizi ya Idomeni katika mpaka kati ya Ugiriki na Makedonia, wakimbizi wakiusubiri kuendelea na safari yao hadi kaskazini (Machi 17, 2016). REUTERS/Alkis Konstantinidis

Ugiriki imesema Jumatatu itaanza zoezi la kuwaondoa wakimbizi katika kambi ya Idomeni kwenye mpaka na Makedonia. Kambi hii imekua ni eneo muhimu kwa maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaokwama kufuatia kufungwa kwa kwa barabara zinazoingia katika nchi za Balkan mwanzoni mwa mwezi Machi.

Matangazo ya kibiashara

Barabara hii imekua ikitumiwa na wahamiaji pamoja na wakimbizi kwa kuingia Ulaya Kaskazini.

Operesheni ya kuwaondo wakimbizi na wahamiaji takriban 8,400 wanaojazana katika kambi hiyo, inatazamiwa kuanza "pengine Jumanne hii," msemaji wa wa Idara ya uratibu wa mgogoro wa uhamiaji nchini Ugriki, Giorgos Kyritsis, ameliambia shirika la habari la Ugiriki la Ana. Tarehe ya Jumatano, hata hivyo,imetajwa na mamlaka ya Ugiriki.

Lakini "haitakua operesheni kabambe ya polisi yenye lengo la kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji kwa siku moja katika kambi ya Idomeni," Bw Kyritsis amesema.

Amebaini kwamba zoezi hili la kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji katika kambi hiyo, lililowezekana baada ya kutengwa siku za hivi karibuni maeneo zaidi ya 6,000 katika vituo vya mapokezi kaskazini mwa nchi, linaweza kuchukua muda wa siku kumi.

Uamuzi wa kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji hao katika kambi hiyo tayari umesababisha watu 400 kukubali Jumapili kuhamishwa katika kituo cha mapokezi karibu na mji wa Thessaloniki wakati ambapo kundi jingine la watu 400 pia limekua likijandaa Jumatatu usiku kufuatana na kundi hilo la kwanza, kwa mujibu wa polisi wa mji wa Idomeni.

"Tunakaribisha mpango wowote wa serikali ya Ugiriki" wa kuwaondoa wakimbizi na wahamiaji katika kambi ya Idomeni, msemaji wa Tume ya Ulaya, Margaritis Schinas, amesema mjini Brussels Jumatatu hii.