Hollande apongeza kuanza vema kwa mashindano
Imechapishwa:
Raisi wa Ufaransa Francois Hollande amepongeza kuanza vema kwa mashindano ya mataifa ya ulaya ya 2016 ijumaa na kushuhudia tishio la mgomo wa wafanyakazi wa vyombo vya usafiri likishindwa kuvuruga michuano nchini humo.
Zaidi ya mashabiki elfu themanini walijitokeza jijini Paris katika mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Ufaransa dhidi ya Romania katika uwanja wa Stade de France,uwanja uliolengwa na mashambulizi ya kigaidi jijini Paris mnamo mwezi Novemba mwaka 2016.
Hata hivyo mashabiki walikuwa katika hali ya amani baada ya majuma ya mgomo wa wafanyakazi na hofu ya tishio la mashambulizi ya kigaidi katika kipindi cha michuano hiyo.
Ulinzi mkali uliimarishwa hususani katika mji wa Marseille ambako kulishuhudia ghasia za mashabiki wa Uingereza na Urusi na kuwarushia chupa maafisa polisi katika usiku wa pili wa vurugu kabla ya mechi ya kwanza kuanza.