EURO 2016-UFARANSA

Vurugu zaenea michuano ya kombe la Ulaya 2016

Mamia ya mashabiki walizunguka mitaani jana Jumamosi wakiwa wamebeba viti vyao kichwani tayari kuvitupa na kujeruhi wanaume waliokuwa vifua wazi wakizozana na polisi, katika vurugu za soka zilizorejea na kisasi nchini Ufaransa

Mashabiki wa Uingereza na Urusi wakipambana katika dimba la  stade Vélodrome jijini Marseille, nchini Ufaransa Jumamosi 11 Juni 2016.
Mashabiki wa Uingereza na Urusi wakipambana katika dimba la stade Vélodrome jijini Marseille, nchini Ufaransa Jumamosi 11 Juni 2016. REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki wa Uingereza na Urusi walipigana vita huko Marseille kabla ya nchi zao kushiriki mechi za uzinduzi wa kombe la Ulaya hapo jana ambapo chupa na viti vya kwenye migahawa vilirushwa na mawingu ya gesi ya kutoa machozi yakatawala wilaya ya Vieux-Port katika jiji hilo.

Chanzo cha polisi kimesema mtu mmoja raia wa Uingereza alipigwa na chuma kichwani na alikimbizwa hospitali baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika eneo la tukio na aliachwa katika hali mbaya na takribani watu 34 walijeruhiwa amesema Laurent Nunez, gavana wa polisi kutoka mji wa kusini mwa Ufaransa.

Vurugu hizo ziliendelea tena katika mechi mwishoni mwa sare ya bao 1-1 huko Stade Velodrome, mashabiki wa Urusi waliwavamia eneo la mashabiki wa Uingereza na vurugu zikazuka.

Baadaye vurugu hizo zilienea katika pwani ya Mediterranian hadi Nice ambapo mashabiki wa Ireland Kaskazini nao waliingia katika mapigano huko Nice jana usiku wakati vurugu za michuano ya kombe la Ulaya zikienea, mashahidi wamesema.

Kwa mujibu wa afisa wa polisi wa Ireland Kaskazini ambaye aliwasindikiza mashabiki katika eneo la tukio, polisi wa Ufaransa wa kutuliza ghasia waliingilia kati baada ya vijana wa Nice kuwarushia chupa mashabiki wa Ireland Kaskazini katika migahawa karibu na Place Massena.

Afisa huyo amesema Karibu vijana 20 hadi 30 wa Nice walianza kurusha chupa kwa mashabiki wa Ireland Kaskazini ambapo baadhi ya chupa zilirushwa tena kwao na makonde kadhaa yalirushwa.

Watu saba walijeruhiwa, akiwemo mwanaume mmoja ambaye alijeruhiwa vibaya kichwani polisi wamesema.

Matukio hayo katika jiji la Marseille yanakumbusha michuano ya kombe la dunia mwaka 1998, Wakati mashabiki wa Uingereza na Tunisia walipopigana katika mji wa bandari katika baadhi ya vurugu mbaya kuwahi kushuhudiwa katika mashindano ya soka.