UFARANSA-MAANDAMANO

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji Paris

Mbinu za polisi wakati wa maandamano dhidi ya sheria ya kazi Alhamisi Mei 26 katika mji wa Paris zimeibua maswali mengi.
Mbinu za polisi wakati wa maandamano dhidi ya sheria ya kazi Alhamisi Mei 26 katika mji wa Paris zimeibua maswali mengi. MATTHIEU ALEXANDRE / AFP

Mamia ya watu waliojificha nyuso zao, leo Jumanne wamekabiliana na vikosi vya usalama, huku wakirusha mawe na vilipuzi wakati wa maandamanao yaliyofanyika mjini Paris dhidi ya sheria ya kazi.

Matangazo ya kibiashara

Watu kumi na tatu walmekamatwa, polisi katika mji wa Paris (PP) imesem. Kwenye akaunti yake ya Twitter, polisi imetoa wito kwa waandamanaji kuajitenga na makundi ya wahuni, ili kuwezesha kuingilia kati kwa vikosi vya usalama.

Katika eneo la Port-Royal, "watu waliingia katika jengo moja ambalo bado linajengwa na kuchukua vifaa vya ujenzi ambavyo walivitumia kwa kurushia vikosi vya usalama, ambavyo vililazimika kuingilia kati", polisi ya mjini Paris imesema.

Polisi wametumia mabomu ya machozi na kuwatimuwa waandamanaji ambao wamekua wakirusha vilipuzi huku wakipiga kelele wakisema "wakazi wa mji wa Paris, simameni, inukeni!" au "kila mtu aichukie polisi". hali hiyo inatokea siku moja baada ya kifo cha askari polisi na mpenzi wake karibu na mji wa Paris katika shambulio la wanajihadi.

Kwa uchache watu wawili wamejeruhiwa, mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP, ameshuhudia.

Vio vya madirisha kadhaa vya benki vimevunjwa na wahuni wakati mwingine wakiungwa mkono na baadhi ya waandamanaji.