UFARANSA-MAUAJI

Ufaransa: afisa wa polisi na mkewe wauawa Yvelines

Gari ya kikosi cha polisi kiliyoendesha operesheniMagnanville, magharibi mwa mji wa Paris, Jumatatu Juni 13 usiku wa manane.
Gari ya kikosi cha polisi kiliyoendesha operesheniMagnanville, magharibi mwa mji wa Paris, Jumatatu Juni 13 usiku wa manane. MATTHIEU ALEXANDRE / AFP

Afisa wa polisi aliuawa kwa kisu Jumatatu usiku nje ya nyumba yake katika kata ya Magnanville wilayani Yvelines, magharibi mwa mji wa Paris, na mtu binafsi, ambaye baadaye alijificha ndani nyumba ya afisa huyo wa polisi. Baada ya muda mchache, urushianaji wa risasi ulianza.

Matangazo ya kibiashara

Muuaji, ambaye alidai kuwa ni mpiganaji wa kundi la Islamic State, alipigwa risasi na kuuawa. Uchunguzi dhidi ya ugaidi umeanzishwa.

Mtu huyo aliyedai kuwa mpiganaji wa kundi la Islamic State alimuua afisa wa polisi kwa kumchoma kisu mara kadhaa nje ya nyumba yake. Baada ya kitendo hiki muuaji huyo alijificha ndani ya nyumba ya afisa huyo wa polisi.

Askari polisi kutoka kitengo cha polisi maarufu wa taifa) waliwasili katika eneo la tukio karibu saa 3:30 usiku na kuweka eneo la usalama kwenye makazi ya mkuu huyo wa polisi. Mazungumzo yalianza na muuaji huyo ambaye alisema kuwa amewashikilia mateka watu kadhaa ndani ya nyumba ya afisa wa polisi aliyeuawa. "Mawasiliano yalifanyika mara kadhaa ili kutatua hali hii," alisema Pierre-Henry Brandet, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Lakini mazungumzo hayo hayakufikia chochote. Muda mchache baadaye milio ya risase na milipuko vilisikika. Wakati huo huo askari polisi waliwasili eneo hilo kwa idadi kubwa na kufaulu kumgamiza muuaji, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa mji wa Versailles.

Baada ya operesheni hiyo askari polisi waliweza kuingia ndani ya nyumba alipokua amejificha muuaji, ambapo walikua mwili wa mke wa mkuu wa polisi aliyeuawa, ambaye alikua Katibu Tawala katika kituo cha polisi cha Mantes-la-Jolie. Mvulana mdogo wa miaka 3, mtoto wa wawili hao waliouawa, alipatikana akiwa salama.

Muuaji adai kuwa mpiganaji wa kundi la Islamic State

Kwa sasa, uraia wala nia ya muuaji havijaweka wazi. Lakini saa chache baada ya tukio hilo, shirika la habari la AMAQ la lenye uhusianao na kundi la wanajihadi lilisema kuwa "mpiganaji wa kundi la Islamic State" alimuua afisa wa polisi na mkewe karibu na mji wa Paris, kwa mujibu wa kituo cha Marekani, SITE, kinachofuatlia tovuti za wanajihadi.

Na kwa mujibu wa vyanzo vya polisi vikinukuliwa na shirika la habari la AFP, mtu huyo aliyeendesha mauaji hayo alidai kuwa mpiganaji wa kundi la Islamic State wakati wa mazungumzo na askari polisi. Mashahidi pia wamewaambia wachunguzi kuwa alipiga kelelea akisema "Allah akbar" alipowashambulia polisi.

Hata hivyo kundi la Islamic State limekiri kuwa mpiganaji wake aliendesha shambulio hilo kwa niaba ya kundi hilo.

Ofisi ya mashitaka dhidi ya ugaidi imeanzisha uchunguzi.

Mkutano katika Ikulu ya Elysee Jumanne asubuhi

Afisa wa polisi aliyeuawa, alikua na umri wa miaka 42, na alikua akihudumu katika kituo cha polisi cha eneo la Mureaux (Yvelines). Rais François Hollande amehakikisha kwamba "mwanga utatolewa" na ameitisha mkutano katika Ikulu ya Elysee Jumanne hii asubuhi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Cazeneuve, ameelezea "huzuni" wake. Ametangaza kuwa atatembelea Jumanne hii asubuhi katika "kituo cha polisi cha eneo la Mureaux na Mantes-la-Jolie" ili "kuonyesha mshikamano wa serikali."