UFARANSA-HOLLANDE

Hollande atishia kupiga marufuku maandamano

Rais wa Ufaransa François Hollande  katika Ikulu ya Elysee, Paris, May 19, 2016.
Rais wa Ufaransa François Hollande katika Ikulu ya Elysee, Paris, May 19, 2016. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Rais François Hollande ametangaza leo Jumatano kuwa maandamano yanaweza kupigwa marufuku katika siku chache zijazo nchini Ufaransa kama ulinzi wa "mali na watu" "hautazingatiwa". Tishio ambalo limepelekea kambi ya mrengo wa kushoto kutoa msimamo wake.

Matangazo ya kibiashara

François Hollande ametoa tangazo hilo katika Baraza la Mawaziri leo asubuhi : kama kutatokea machafuko mapya, na ulinzi wa "mali na watu" kutozingatiwi, bila shaka maandamano yatapigwa marufuku. Msemaji wa serikali, Stéphane Le Foll, anesema kwa vyombo vya habari.

"Katika wakati ambapo Ufaransa inapokea michuano ya Kombe la Ulaya, ambapo Ufaransa inakabiliwa na ugaidi, hakutakua na ruhusa yoyote ya kuandamana iwapo masharti ya ulinzi wa mali na watu havitozingatiwa", amesema Rais Hollande.

Jana, Jumanne, maandamano mapya dhidi ya sheria ya kazi yaligubikwa na vurugu. Mamia kadhaa ya wahuni walikabiliana na vikosi vya usalama katika eneo la Seine, mjini Paris, na kusababisha uharibifu mkubwa.

"Wakataze michuano ya Kombe la Ulaya! "

Tishio la rais wa nchi ya Ufaransa limepelekea pande mbalimbali kutoa hisia zao. Kiongozi wa chama cha wafanyakazi, Jean-Claude Mailly, amepinga kauli hiyo ya rais, akipendekeza kwamba kama ni hivyo, "wakataze michuano ya soka Kombe la Ulaya kwani inakabiliwa pia na vurugu."

François Hollande "anakiuka sheria ya Katiba ya kuandamana, ametuhumu kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha CRC katika Baraza la Seneti, Eliane Assassi.