UINGEREZA-EU-COX

Serikali ya Uingereza yahuzunishwa na mauaji ya Mbunge Jo Cox

serikali ya Uingereza na vyama vya kisiasa wapigwa na butwaa baada ya polisi kutangaza kifo cha Mbunge Jo Cox, Alhamisi Juni 16, 2016.
serikali ya Uingereza na vyama vya kisiasa wapigwa na butwaa baada ya polisi kutangaza kifo cha Mbunge Jo Cox, Alhamisi Juni 16, 2016. DANIEL LEAL-OLIVAS / AFP

Polisi ya Uingereza imetangaza Alhamisi hii mchana, kifo cha Mbunge Jo Cox, aliyeshambuliwa siku hiyo hiyo kaskazini mwa Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Ingawa mazingira ya shambulizi hili bao hayajawekwa wazi, mashuhuda wanasema kwamba Jo Cox alishambuliwa barabarani na mtu mwenye umri wa miaka 52 ambaye alitumia bunduki ya kwa kummalizia maisha Mbunge huyu, aliyekua katika kambi ya Waingereza wanaotetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, Jo Cox, baada ya kupigwa risasi kadhaa alichomwa kisu akiwa katika hali mbaya.

Jo Cox, Mbunge kutoka Uingereza, mwenye umri wa miaka 41alijeruhiwa kwa risasi wakati alipokua akikutana na wafuasi wake katika jimbo lake. Baada ya kupigwa risasi, Jo Cox alidondoka kati ya magari mawili madogo madogo, mmoja wa mashahidi amesema.

Inasemekana kwamba Jo Cox aliingilia kati wakati watu wawili walikua wakipigana. Jo Cox alisafirishwa hospitali akiwa katika hali mbaya, kaskazini mwa nchi.

Kufuatia kisa hiki cha kushambuliwa kwa Mbunge huyo, kambi inayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya ilitangaza mapema Alhamisi mchana kwamba inasimamisha kampeni zake dhidi ya nchi hiyo kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

Shambulizi hili limetokea wiki moja kabla ya kura ya maoni juu kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Kufuatia kitendo hicho, kampeni dhidi ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya imesimamishwa. Kwenye Twitter, David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza, amesema anatiwa "wasiwasi", akiongeza kuwa "katika mawazo yetu na sala zetu tuko pamoja na Jo na familia yake."

Hisia mbali mbali zimeanza kutolewa

Vyama vya kisoisa nchini Uingereza vimelaani shambulio hilo lilisababisha kifo cha Mbunge Jo Cox. Vyama hivyo vimeomba uchunguzi kuanzishwa ili kujua waliohusika na kifo hicho na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kwenye akaunti yake ya Twitter: "Kifo cha Jo Cox ni janga. Alikuwa Mbunge shujaa na anayestahili. Salamu zangu za rambi rambi zimuendee mumewe Brendan na watoto wake wawili wadogo. "