UINGEREZA

Mtuhumiwa wa mauaji ya mbunge Jo cox kufikishwa kizimbani hii leo

Pichani ni mbunge wa chama cha Labour Jo Cox enzi za uhai wake
Pichani ni mbunge wa chama cha Labour Jo Cox enzi za uhai wake 路透社

Mtuhumiwa mkuu Thomas Mair ameshitakiwa kwa mauaji ya mbunge wa Uingereza Jo Cox na atafikishwa mahakamani baadaye leo Jumamosi, polisi imesema.

Matangazo ya kibiashara

Cox alishambuliwa kwa kisu na silaha ya moto nje ya jimbo lake katika kijiji cha Bristall, Kaskazini mwa Uingereza siku ya Alhamisi.

Mauaji yake yametuma hofu katika siasa za Uingereza na salamu za rambirambi kutoka duniani kote, ambapo Rais wa Marekani Barack Obama amelaani vikali shambulio hilo.

Kampeni za mwisho kabla ya kura ya maoni siku ya alhamisi kuhsuu Uingereza kujiondoa au kubaki kwenye umoja wa Ulaya zimeendelea kusitishwa leo Jumamosi kama ishara ya heshima kwa mbunge huyo.

Mair mwenye umri wa miaka 52, kutoka katika kijiji tulivu cha Birstall,katika vilima vya Yorkshire, alikamatwa Alhamisi karibu na eneo la mashambulizi.

Polisi wa Upelelezi Magharibi mwa Yorkshire Nick Wallen, ambaye ni kiongozi wa uchunguzi, amesema katika taarifa fupi kwamba Mair amewahi kushtakiwa kwa uhalifu uhalifu kadhaa unaohusiana na kifo mbunge wa chama cha Labour.