UFARANSA-EURO 2016

Euro 2016: vikosi vya usalama na ulinzi vyatoa ulinzi wa kutosha

Vikosi vya usalama na ulinzi vikiwa tayari kutoa ulinzi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya michuano ya Kombe la Ulaya (Euro 2016).
Vikosi vya usalama na ulinzi vikiwa tayari kutoa ulinzi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya michuano ya Kombe la Ulaya (Euro 2016). AFP/ Jacques DEMARTHON

Vikosi vya usalama vimefanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi watu kati ya 557 na 344 tangu kuanza kwa michunao soka ya Kombe la Ulaya, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, ametangaza Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Siku kumi baada ya kuanza kwa michuano hiyo, Bernard Cazeneuve amesema kuwa mashabiki 21 walifukuzwa, kulitangazwa "uamuzi mkali wa kifungo kwa idadi ya mashabiki kadhaa wanaochochea na kuhusika katika vurugu", pamoja na uwezekano kuondoka katika ardhi ya Ufaransa.

Askari na askari polisi 70,000 walitumwa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya tukio hili muhimu, ambapo nusu ya mechi tayari zimechezwa, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa amekumbusha.