UNHCR-WAKIMBIZI

Siku ya Kimataifa ya wakimbizi 2016: taarifa yetu maalum

Wanawake na watoto wakimbizi wanapanga foleni kwa ajili ya kupata chakula karibu na kijiji cha Idomeni kwenye mpaka wa Ugiriki na Makedonia Aprili 21, 2016.
Wanawake na watoto wakimbizi wanapanga foleni kwa ajili ya kupata chakula karibu na kijiji cha Idomeni kwenye mpaka wa Ugiriki na Makedonia Aprili 21, 2016. REUTERS/Stoyan Nenov

Juni 20 ni Siku ya Wakimbizi Duniani. Tarehe hii inakwenda na sanjari na kupitishwa kwa Mkataba wa 1951 unaohusu sheria ya wakimbizi.

Matangazo ya kibiashara

Kila mwaka tangu mwaka 2001, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limekua likitafuta kuhimiza kuhusu uelewa wa sababu ya wanadamu hizi. Folder.

Mwaka 2015, watu milioni 65.3 walilazimishwa kukimbia makazi yao kwa sababu ya vita au mateso. Idadi hii imevunja rekodi. Miongoni mwa wat hao, zaidi ya milioni 40 ni wakimbizi wa ndani. Kwa maneno mengine, watu walibaki waliokimbia makazi yao lakini hawakuweza kuvuka mpaka na kukimbilia nchi za nje. Na milioni 21.3 ni wakimbizi, ni kusema walilazimika kukimbiloia nje ya nchi zao.

■ Antonio Guterres, aliyekuwa Kamishna wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi, amejibu maswali ya RFI. aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ureno, mgombea katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anaona "kushindwa kwa kiasi kikubwa kwa jumuiya ya kimataifa, katika kuzuia migogoro ya kisiasa na utatuzi wa migogoro."

■ Zaidi ya wakimbizi 32,000 wa Mali, sasa wanaishi nchini Burkina Faso. Tangu mwaka 2012, wakimbizi hao walikimbia vita kati ya waasi wa kaskazini na serikali ya Bamako. Kwa kuzingatia hali ya wakimbizi hawa, hawako tayari kurudi nchini mwao.

■ MSF inawasaidia maelfu ya wakimbizi wa Eritrea katika makambi kadhaa kaskazini mwa Ethiopia. Baadhi wamekuwa katika makambi hayo kwa miaka mingi. Maelfu bado wameendelea kuwasili kila mwezi.

■ Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, zaidi ya wakimbizi 18,000 kutoka Burundi wanaishi katika kambi ya mapokezi ya Lusenda, ilifyoungua mwaka mmoja na nusu uliyopita. Miongoni mwao, kuna sehemu kubwa ya watoto.

■ Kusini mashariki mwa Niger, karibu wakimbi 300 000 na wakimbizi wa ndani wameorodheshwa, bila kuhesabu watu wengi wanaopokelewa na familia mbalimbali. Hali haitoboreka, ka sababau wapiganaji wa Boko Haram wanaendelea na mashambulizi makubwa. Hivi karibuni: Jun mji wa Bosso, mji mwa Ziwa Chad, ulishambuliwa na kulazimisha raia 50,000 kukiyambia makazi yao.

■ Katika Amerika ya Kati, watu zaidi na zaidi wanakimbia vurugu zinazohusiana na madawa ya kulevya na silaha na kukimbilia katika nchi jirani, kama Marekani. Andrés Ramirez, UNHCR Mwakilishi wa Mkoa kwa ajili Amerika ya Kati, ameilezaa ufumbuzi RFI ulioanzishwa ili kuboresha hali ya wakimbizi.

■ Paris imekuwa kupitishia maelfu ya wahamiaji, hasa katika wilaya za kaskazini mwa mji mkuu wa Ufaransa. mkutano wa hadhara umepangwa Jumatatu hii Juni 20 katika eneo la Jamhur. Kwa vyama ambavyo huwasaidia wakimbizi, mamlaka hawapendekezi ufumbuzi wa kweli kwa ajili ya mapokezi yao.