UINGEREZA-EU

Siku moja kabla ya kura ya maoni, juhudi zaendelea

Boris Johnson, Mkuu wa zamani wa jiji la London, akionyeshwa kwenye televisheni kubwa Wembley mjini London, wakati wa mjadala mkubwa Jumanne, 21 Juni 23 Juni kabla ya kura ya maoni.
Boris Johnson, Mkuu wa zamani wa jiji la London, akionyeshwa kwenye televisheni kubwa Wembley mjini London, wakati wa mjadala mkubwa Jumanne, 21 Juni 23 Juni kabla ya kura ya maoni. Jeff Overs/Courtesy of the BBC

Hotuba, mahojiano, mjadala na harakati mbalimbali zimekua zikiendeshwa na kambi mbili tofauti nchini Uingereza siku moja kabla ya kura ya maoni kuhusu kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Siku moja kabla ya kura hii muhimu ya maoni kwa ajili ya mustakabali wa nchi ya Uingereza lakini pia mustakabali wa Umoja wa Ulaya, zimekua zikikaribiana kwa kura kulingana na uchunguzi uliyoendeshwa mashirika mbalimbali pamoja na vyombo vya habari vya Uingereza. Upande wa kambi inayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya wamefikia sasa 51% kwa mujibu wa wastani wa uchunguzi wa mwisho uliyoendeshwa na tovuti ya WhatUKThinks.

Lengo liko wazi kwa pande zote mbili: inabidi kuwashawishi wapiga kura % 10 ambao wanaweza kupelekea kufikia idadi ya juu inayohitajika kila upande.

Waziri Mkuu kutoka chama cha Conservative, David Cameron alitoa maoni yake katika mahojiani yaliyochapishwa kwenye ukurasa wa mwanzo wa gazeti la kila wiki la Guardian. Bw Cameron amesema kuwa kuchagua kubaki kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, wapiga kura watatuma "ujumbe wa wazi" kwamba Uingereza itanufaika katika sekta mbalimbali."

Jumanne jioni, maofisa kadhaa kutoka pande zote mbili walikuwa pia wakijaribu kuwashawishi wapiga kura katika mjadala uliyoandaliwa nashirika la utangazaji la BBC mbele ya watu 6,000 katika ukumbi wa michezo mjini London, nchini Uingereza.