UINGEREZA-EU

Kambi inayotaka Uingereza kuondoka katika EU yaongoza

Zoezi la kuhesabu kura katika mji wa Glasgow, Scotland.
Zoezi la kuhesabu kura katika mji wa Glasgow, Scotland. REUTERS/Clodagh Kilcoyne

Kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya na ile inayotaka nchi hiyo kuondoka katika umoja huo zimekua zikisogeleana kwa kura katika usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa hii baada ya kutangazwa kwa matokeo ya awali.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo rasmi ya kura hii ya maoni kwa madhara makubwa kwa mustakabali wa Uingereza na maeneo mengine ya Ulaya yatatangazwa Ijumaa hii asubuhi.

Matokeo ya kura ya maoni hatarishi ya Alhamisi hii yanaendelea kutangazwa nchini Uingereza. Inasadikiwa kuwa kiwango cha ushiriki kilikua juu ya 70% wakati ambapo zoezi la kuhesabu kura linaendelea majimbo kwa majimbo, huku wafuasi wa kambi zote mbili wanaonekana kila upande kuwa na hamu ya kujua matokeo ya kura hii ya maoni.

Wakati ambapo Alhamisi hii usiku, utafiti wa sera na masoko ulikua unaipa ushindi mdogo kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, matokeo ya kwanza, katika neema ya kambi inayotaka Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya, yameongeza mashaka ya kura hii ya maoni.

Baada ya kuhesabu kura katika maeneo 200 kwa jumla ya maeneo 382, kambi inayotaka Uingereza kuondoka katik Umoja wa Ulaya inaongoza kwa 51.7% ya kura, kulingana na matokeo rasmi.

Matokeo ya kwanza

Newcastle mji mkubwa wa kwanza kwa kutangaza matokeo yake, umepiga kura katika neema ya kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya kwa 50.7% ya kura wakati ambapo kambi inayotaka nchi hiyo kuondoka katika Umoja wa Ulaya imepata 49.3% ya kura.

Na Sunderland, mji mwingine wa kaskazini mwa Uingereza, kwa upande wakazi wake wengi wamepiga kura katika neema ya kambi inayotaka Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa zaidi ya 61% ya kura.

Katika eneo la Gibraltar hata hivyo, wakazi wa eneo hilo wamepiga kura kwa katika neema ya kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya kwa zaidi ya 95% ya kura, amesema kiongozi wa zoezi la kuhesabu kura katika eneo hilo, ambaye alikua wa kwanza kutangaza matokeo.