EU-UINGEREZA

Scotland: Tutafanya kura yetu ya maoni, sahihi milioni 1 zapatikana

Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Paolo Gentilon na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, wakiteta kando na mkutano wao wa hapo jana mjini Berlin.
Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Paolo Gentilon na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, wakiteta kando na mkutano wao wa hapo jana mjini Berlin. REUTERS/Axel Schmidt

Waziri wa kwanza wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema ataomba kufanyika haraka kwa mjadala na wakuu wa Brussels ili kuilinda nchi yake kwenye mkataba wa umoja wa Ulaya, baada ya nchi ya Uingereza kupiga kura ya kuachana na jumuiya hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza punde baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa baraza lake la mawaziri, Sturgeon amesema, wamekubaliana kuomba mjadala wa dharura na taasisi za umoja huo pamoja na nchi nyingine wanachama, kuangalia uwezekano wa nchi yake kulindwa na kupewa nafasi ndani ya umoja wa Ulaya.

Nchi ya Uingereza kwa ujumla imepiga kura kwa asilimia 52 kwa asilimia 48 kuondoka kwenye jumuiya ya Ulaya, katika tukio la kihistoria la kura ya maoni nchini humo. Lakini Scotland ilipiga kura kwa nguvu Uingereza kusalia kwenye umoja wa Ulaya kwa asilimia 62 dhidi ya 38.

Siku ya Ijumaa, Sturgeon alisema kuwa matokeo ya kura ya maoni Uingereza kujitoa kwenye umoja wa Ulaya, yametoa nafasi ya kufanyika upya kwa kura ya maoni kutaka uhuru wa Scotland, na kwamba huenda kura hiyo ikafanyika ndani ya miaka miwili ijayo.

MATUKIO KATIKA PICHA YA UINGEREZA KUTAKA KUJITOA UMOJA WA ULAYA

Aligusia kipendele kilichoko kwenye ilani ya chama chake, kwamba kuna uwezekano na umuhimu mkubwa wa kutokea mabadiliko, kipengele ambacho kilishuhudia Scotland ikipiga kura ya kutaka kujitenga mwaka 2014, ambapo asilimia 55 walitaka nchi yao isalie chini ya Uingereza.

Katika hatua nyingine, maombi mapya ya kufanyika kwa kura nyingine ya maoni kuhusu uanachama wa nchi ya Uingereza kwenye umoja wa Ulaya, yamepata saini zaidi ya milioni moja.

Maombi haya mapya sasa yatajadiliwa bungeni kama sheria inavyotaka kwakuwa, sahihi zaidi ya milioni moja zimepatikana kuomba kura mpya kufanyika.

Nchi ya Uingereza ilipiga kura kuondoka kwenye jumuiya ya Ulaya kwa asilimia 52 kwa 48, lkini watu wengi kwenye jiji la Londo, Scotland na Ireland Kaskazini walipiga kura kuunga mkono nchi yao kusalia.

Kufuatia kura hiyo, waziri mkuu David Cameron amesema atajiuzulu nafasi yake ifikapo mwezi October kupisha waziri mkuu mpya atakayesimamia mchakato wa nchi hiyo kujitoa.

Kwa upande mwingine, mawaziri wa nchi waasisi wa umoja wa Ulaya waliokutana mjini Berlin, wamekubaliana kuweka shinikizo zaidi kwa nchi ya Uingereza kuharakisha kujitoa kwenye jumuiya yao.