UINGEREZA-EU

Uingereza yapigwa marufuku kuhudhuria mkutano wa EU

Donald Tusk (kushoto), Rais wa Baraza la Ulaya akizungumza na Mwenyekiti wa tume ya Ulaya,  Jean-Claude Junkcer, Februari 17, 2016 Brussels.
Donald Tusk (kushoto), Rais wa Baraza la Ulaya akizungumza na Mwenyekiti wa tume ya Ulaya, Jean-Claude Junkcer, Februari 17, 2016 Brussels. REUTERS/Yves Herman

Nchi ya Uingereza imepigwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya. Kwa sasa mkutano huo utakua ukihudhuriwa na viongozi kutoka nchi 27 badala ya 28, baada ya Uingereza kuamua hivi karibuni kujitoa katika Umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umemshangaza Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ambaye ametakiwa kutokuwepo wakati viongozi 27 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya watakuwa wakikutana katika kikao kisio rasmi juu ya mustakabali wa muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza.

Baraza la Ulaya lilikutana Jumanne hii, baada ya Uingereza kuamua kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, katika muktadha wa kutafakari jinsi ya kuimarisha uchumi, maendeleo na ushirikiano katika umoja huo.

Jumatatu wiki hii Juni 27, Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi walikutana mjini Berlin kwa maandalizi ya mkutano wa Baraza la ulaya ambao ulifanyika Jumanne hii mjini Brussels. Viongozi hao watatu walitoa kauli mmoja ya kupinga mazungumzo na London kabla ya kurasimisha uamuzi wake wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Angela Merkel, François Hollande na Matteo Renzi wameonyesha msimamo pamoja dhidi ya kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Viongozi hao walithibitisha hayo walipokutana Jumatatu hii mjini Berlin. Walisema hakutakuwa na mazungumzo na London kama Uingereza itakua bado haijarasimisha ombi lake la kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kwa Baraza la Ulaya.

Rais wa Umoja wa Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa shughuli za kutegua kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano huo zinapaswa kutekelezwa baada tu ya Uingereza kumpata Waziri Mkuu mpya.