UTURUKI

Watu zaidi ya 34 wapoteza maisha kwenye shambulio la bomu Istanbul

Watu 36 wameripotiwa kufa na wengine mamia wamejeruhiwa baadaya kutekelezwa kwa mashambulizi matatu ya kujitoa muhanga yaliyofuatiwa na makabiliano ya risasi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk jijini Instanbul Uturuki.

Mamia ya abiria na raia wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Istanbul baada ya shambulio la bomu
Mamia ya abiria na raia wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Istanbul baada ya shambulio la bomu REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Serikali inasema waliohusika ni wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic state walioko nchini Syria, ambapo inadaiwa washambuliaji walianza kwa kufyatua risasi kulenga geti la kuingia abiria wanaoondoka kabla ya kujilipua.

Hili ni shambulio baya la nne kufanywa katikati mwa jiji kuu la Uturuki, Instanbul kwa mwaka huu, ambapo mashambulizi mengine yaliyotekelezwa kundi la Islamic State lilinyooshewa kidole huku moja likidaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Kikurdi.

Licha ya kuwa kundi la Islamic State halijasema ikiwa limehusika kwenye shambulio hili la usiku wa kuamkia leo, waziri mkuu wa nchi hiyo, Binali Yildirim, amewaambia waandishi wa habari kuwa, ushahidi wote unaonesha kuwa walikuwa wapiganaji wa ISIL.

Wataalamu wa vinasaba wakifanya uchunguzi nje ya jengo la kuingilia abiria kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Istanbul, Uturuki, 29 juni 2016
Wataalamu wa vinasaba wakifanya uchunguzi nje ya jengo la kuingilia abiria kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Istanbul, Uturuki, 29 juni 2016 REUTERS/Murad Sezer

Waziri wa sheria nchini Uturuki, Bekir Bozdag, amesthibitisha kutokea kwa vifo hivyo, ambapo amesema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na raia wa kigeni, huku akitaja idadi ya waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo kuwa ni 147.

Shambulizi hili la kupangwa na kundi la Islamic State, linafuatia mashambulizi kama hayo yaliyofanywa jijini Brussels kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni ambapo watu zaidi ya 32 waliuawa.