UINGEREZA-EU

Theresa May yuko kwenye nafasi nzuri ya kumrithi Cameron

Waziri wa mambo ya Ndani wa Uingereza Theresa May yuko kwenye nafasi nzuri, Ijumaa hii, katika mbio za kumrithi David Cameron, kwenye nafasi ya Waziri Mkuu, baada ya uamuzi wa Boris Johnson, kutangaza kutowania kwenye nafasi ya Waziri Mkuu.

Theresa May anapewa nafasi kubwa ya kumrithi david Cameron.
Theresa May anapewa nafasi kubwa ya kumrithi david Cameron. REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Boris Johnson ni kiongozi wa kambi ya waliokua wakitetea Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Kwa jumla wagombea watano ndio wanashiriki mbio hizo, ispokua, Boris Johnson, aliyekua amepewa nafasi ya kushinda, ambaye alitangaza Alhamisi kwamba alijiondoa katika kinyang'anyiro.

"Ninataka kuwawambia marafiki zangu, kwamba nyinyi mnaosubiri kauli ya mshangao, naamua kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Waziri Mkuu," Johnson amesema.

Uamuzi huu uliwashangaza wengi. Kwa sababu hata kama mkuu huyo wa zamani wa jiji la London alipongezwa tangu ushindi wa wanaounga mkono kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, hakuna mtu ambaye alitarajia kuwa Bw Johnson atachukua uamuzi baada ya wiki.

Boris Johnson alichukulia kuuwania kwa Waziri wa Sheria Michael Gove, mwenye umri wa miaka 48, alhamisi hii kama usaliti.

Theresa May, ambaye ana wasifu wa kuunganisha chama hata kama alikuwa akishirikiana na David Cameron kwa kutetea Uingereza kubaki katik Umoja wa Ulaya pia anataka ni miongoni mwa wagombea watakaopigiwa kura Septemba 9 kwa minajili ya kumrithi david Cameron.