UINGEREZA-EU-DAVID CAMERON

Uingereza kuwa na Waziri Mkuu mwanamke

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk Septemba 24, 2015 jijini Brussels.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya Donald Tusk Septemba 24, 2015 jijini Brussels. AFP/AFP

Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri Mkuu mwanamke, wa kwanza baada ya Waziri Mkuu wa zamani Margaret Thatcher. Hii ni mara ya pili Uingereza kuwa na Waziri Mkuu mwanamke katika historia yake

Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika baafa ya chama tawala cha Conservative kuwachagua wanasiasa wawili wanawake, Theresa May na Andrea Leadsom kuwania wadhifa huo baada ya Waziri Mkuu wa sasa David Cameron kutangaza kuwa atajiuzuliu kabla ya mwezi Oktoba baada ya raia wa Uingereza kuamua kujiodnoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Wawili hao sasa watapambana kuwania Uenyekiti wa chama chao kwa kupigia kura na zaidi ya wajumbe 150,000 na mshindi atatangazwa tarehe 9 mwezi Septemba.
Theresa May ni Waziri wa Mambo ya ndani huku Andrea Leadsom akiwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati.

Itafahamika kwamba Waziri Mkuu David Cameron alitangaza hivi karibuni uamuzi wake wa kujiuzulu, baada ya raia wa Uingereza kupiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

David Cameron alikua katika kambi iliyokua ikitetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, lakini akambi yake ilionekana kushindwa baada ya kambi iliyokua ikitaka Uingereza kujiondoka katika Umoja huo kupata ushindi mkubwa.