UINGEREZA-EU-THERESA MAY

Theresa May mgombea pekee kwenye nafasi ya Waziri Mkuu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Theresa May, mbio kua mwanamke wa pili kushikilia nafasi ya Waziri Mkuu nchini Uingereza baada ya  Margaret Thatcher.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Theresa May, mbio kua mwanamke wa pili kushikilia nafasi ya Waziri Mkuu nchini Uingereza baada ya Margaret Thatcher. REUTERS/Andrew Yates

Andrea Leadsom ameamua kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Waziri Mkuu nchini Uingereza na kuhakikisha kwamba Theresa May yuko "kwenye nafasi nzuri" ya kushinda.

Matangazo ya kibiashara

"Kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ina maana hiyo hiyo" na "tutapata mafanikio", Theresa May amesema mapema asubuhi, akiwa ni mgombea pekee kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu. Theresa May amethibitisha kwamba hakutakuwa na "jaribio lolote la kubaki katika Umoja wa Ulaya."

Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri Mkuu mwanamke, wa kwanza baada ya Waziri Mkuu wa zamani Margaret Thatcher. Hii ni mara ya pili Uingereza kuwa na Waziri Mkuu mwanamke katika historia yake.

Chama tawala cha Conservative kiiiwachagua wanasiasa wawili wanawake, Theresa May na Andrea Leadsom kuwania wadhifa wa Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu wa sasa David Cameron kutangaza kuwa atajiuzuliu kabla ya mwezi Oktoba.

Theresa May ni Waziri wa Mambo ya ndani huku Andrea Leadsom akiwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati.

Itafahamika kwamba Waziri Mkuu David Cameron alitangaza hivi karibuni uamuzi wake wa kujiuzulu, baada ya raia wa Uingereza kupiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

David Cameron alikua katika kambi iliyokua ikitetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, lakini akambi yake ilionekana kushindwa baada ya kambi iliyokua ikitaka Uingereza kujiondoka katika Umoja huo kupata ushindi mkubwa.