ITALIA-AJALI

Italia: watu wasiopungua 12 wapoteza maisha katika ajali ya treni

Watu kumi na mbili wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana kusini mwa Italia, katika mkoa wa Apulia, Idara ya mawasiliano ya mkoa huo imeliambia shirika la habari la AFP.

Jumanne, Julai 12, 2016, treni mbili za abiria zimegongana katika mkoa Apulia (kusini).
Jumanne, Julai 12, 2016, treni mbili za abiria zimegongana katika mkoa Apulia (kusini). Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Watu kumi na mbili wamepoteza maisha, ni rasmi, na kuna labda watu wawili walioongezakakwenye idadi hiyo," Idara ya mawasiliano ya mkoa wa Apulia imesema.

vyombo vya habari kadhaa vimearifu kuwa watu 20 wamepoteza maisha, vikimnukuu Makamu wa rais wa mkoa, Giuseppe Corrado, lakini hakuna chanzo kingine kilikua na uwezo wa kuthibitisha rasmi idadi hii mapema mchana.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika watu thelathini wamejeruhiwa, wengi wakiwa katika hali mbaya.

Viongozi katika mkoa huo wametoa wito kwa wahisani kuja kutoa damu na wameitisha madaktari na wauguzi wote walioko katika likizo, kufuta shughuli zote zisizokuwa za dharura katika hospitali.