UINGEREZA-EU-THERESA MAY

Theresa May atawazwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza

Theresa May wakati wa hotuba yake baada kuteuuliwa rasmi kama Waziri Mkuu na Malkia tarehe 13 mwezi Julai.
Theresa May wakati wa hotuba yake baada kuteuuliwa rasmi kama Waziri Mkuu na Malkia tarehe 13 mwezi Julai. REUTERS/Peter Nicholls

Theresa May ametawazwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Jumatano hii na kutakiwa na Malkia Elizabeth II kuunda serikali mpya itakayokua na kibarua kigumu cha kutekeleza uamuzi wa wananchi wa Uingereza wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Theresa May amesisitiza haja ya kupambana dhidi ya dhulma ya kijamii na amebaini kwamba kipaumbele chake sio matajiri, wenye nguvu na wale wenye kuwa nafasi za juu lakini wafanyakazi wanaotambua majukumu yao, huku akiaapa kuwasaidia kupata udhibiti zaidi kwa maisha yao. Kiongozi huyo mpya pia ameahidi kuimarisha Uingereza na kuhifadhi uhusiano kati ya mataifa manne yanayounda utawala wa kifalme.

Hatimaye Theresa May, bila shaka, ameweka wazi changamoto kubwa zinazoikabili nchi ya Uingereza baada ya kura ya maoni ya Uingereza kujiondoka katika Umoja wa Ulaya, akielezea kuwa anataka "nchi izidishe ujasiri na jukumu chanya duniani."

Kazi ngumu

Theresa May, mwenye umri wa miaka 59, ni mwanamke wa pili kushikilia wadhifa wa Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya Margaret Thatcher, na anajulikana kwa uamuzi wake, ujasiri wake katika utendaji wake na amethibitisha hadharani nia yake ya kuendelea kuboresha Chama cha Conservative, mchakato ulioanzishwa na David Cameron .

Theresa May ametangaza uteuzi wa mshirika wake Philip Hammond kama Waziri wa Fedha. Meya wa zamani wa London mtetezi mkuu wa kambi iliyokua ikitetea Uingereza kujionda katika Umoja wa Ulaya, Boris Johnson, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.