MAREKANI-DONALD TRUMP

Donald Trump aahirisha mkutano wake na waandishi wa habari

Mgombea urais katika kura za mchujo kwa chama cha Republican, Donald Trump, katika kampeni Eugene katika jimbo la Oregon, Mei 6, 2016.
Mgombea urais katika kura za mchujo kwa chama cha Republican, Donald Trump, katika kampeni Eugene katika jimbo la Oregon, Mei 6, 2016. REUTERS/Jim Urquhart

Donald Trump, mgombea urais wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais nchini Marekani uliopangwa kufanyika Novemba 8, ameahirisha mkutano na waandishi wa habari uliokua umepangwa kufanyika Ijuma hii kwa sababu ya tukio la mjini Nice, Donald Trump amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Dereva wa lori aliingiza kwa kasi lori lake katika umati wa watu waliokua wakitazama urushwaji wa fataki katika maadhimisho ya Siku kuu ya kitaifa ya Julai 14 nchini Ufaransa, katika eneo la Promenade des Anglais na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80.

Donald Trump aliwafahamisha Alhamisi wiki hii viongozi wa chama cha Republican kwamba amemchagua Mkuu wa jimbo la Indiana, Mike Pence, kuwa mgombea mwenza wake, vyanzo vilio karibu na chama cha Republican vimebaini.

Jason Miller, msemaji wa kampeni za Donald Trump, amesema Donald Trump bado hajachukua uamuzi.