UFARANSA-AJALI-MAUAJI

Watu wasiopungua 80 wauawa katika shambulio Nice

Wanajeshi na askari polisi watoa ulinzi katika eneo la Promenade des Anglais, baada ya shambulio lililosababisha vifo vya watu wengi, lilitokea Julai 14, 2016 Nice.
Wanajeshi na askari polisi watoa ulinzi katika eneo la Promenade des Anglais, baada ya shambulio lililosababisha vifo vya watu wengi, lilitokea Julai 14, 2016 Nice. REUTERS/Eric Gaillard

Kwa uchache watu 80 wamepoteza maisha Alhamisi usiku katika mji wa Nice baada ya kugongwa na lori lililoingizwa kwa kasi katika katika umati wa watu kwenye umbali wa kilomita 2, kwa mujibu wa Christian Estrosi, Mwenyekiti wa Baraza la kimkoa la PACA na meya wa zamani wa Nice.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea alhamisi usiku wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku kuu ya kitaifa ya Julai 14. Watu zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

"Idadi hii bado ni ya muda, " ameongeza mwendesha mashtaka wa Nice, Jean-Michel Pretre. Ofisi ya mashtaka imekabidhi kesi hiyo kitengo kinachopamabana na ugaidi cha Ofisi ya mashitaka ya mjini Paris kwa kuanzisha anzisha uchunguzi waliokabidhiwa sehemu za kupambana na ugaidi wa mwendesha Paris.

Kitendo cha ugaidi kigaidi kinashukiwa, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na uchunguzi. Na chanzo cha polisi, kinabaini kwamba bunduki angalau moja imekutwa ndani ya lori.

Tukio hilo limetokea wakati ambapo maelfu ya watu walikua wakikusanyika ili kutazama urushwaji wa fataki katika eneo la Promenade des Anglais mjini Nice. Kwa mujibu wa mashahidi katika eneo hilo, lori nyeupe liliingizwa kwa kasi katika umati wa watu saa 4:30 saa za Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Ndani amesema watu 80 wamepoteza maisha na wengine 18 wako katika hali mbaya.

Mashahidi wanasema wakati huohuo milio ya risasi ilisikika kutoka upande wa kori. "Hata hivyo dereva wa lori hilo aliuawa," amesema Sébastien Humbert.