UTURUKI-USALAMA

Wafuasi wa Erdogan waandamana kumuunga mkono

Wafuasi wa raisi Erdogan wakiandamana Instanbul 16 Juillet 2016.
Wafuasi wa raisi Erdogan wakiandamana Instanbul 16 Juillet 2016. REUTERS/Huseyin Aldemir

Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza mitaani nchini Uturuki kumuunga mkono raisi wa taifa hilo Recep Tayyip Erdogan,baada ya mamlaka kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya kijeshi ambalo liligharimu maisha ya takribani watu 265.

Matangazo ya kibiashara

Erdogan kwa kujiamini aliwahutubia wafuasi wake jijini Instanbul waliokuwa wakipeperusha bendera za taifa hilo.
Mamlaka zimeelekeza kidole cha lawama kwa Fethullah Gulen,muhubiri raia wa Marekani ambaye ni hasimu wa Erdogan kwa kupandikiza jaribio la mapinduzi hayo ya kijeshi.
Siku ya jumamosi Televisheni za uturuki zilionesha askari lukuki wakijisalimisha baada ya kushindikana kwa jaribio la mapinduzi wengine wakiwa wameweka mikono yao nyuma ya vichwa.

Kundi hilo la kijeshi kuanzia Ijumaa usiku limekuwa likijaribu kuchukua madaraka baada ya makabiliano makali jijini Ankara, Istanbul na miji mingine.

Kaimu Mkuu wa jeshi Jenerali Umit Dundar ametangaza kuwa watu 104 waliopanga mapinduzi hayo wameuawa huku wengine 1,563 wakikamatwa.