UFARANSA-USALAMA

Seneti yapitisha ombi la serikali la kuongezwa muda wa hali ya hatari

Maseneta wapiga kura ya kuongezwa muda wa hali ya hatari Jumatano jioni Julai 20.
Maseneta wapiga kura ya kuongezwa muda wa hali ya hatari Jumatano jioni Julai 20. AFP PHOTO / ALAIN JOCARD

Nchini Ufaransa, Maseneta walipitisha Jumatano hii Julai 20 nakala inayoeleza kuongezwa muda wa hali ya hatari baada ya kuifanyia ikilinganishwa na ile iliyopigiwa kura na Wabunge siku moja kabla.

Matangazo ya kibiashara

Mjadala wa kipeke uliongezwa kwa mkutano wa kamati ya pamoja, kundi la wabunge linalohusika na kuwaweka sawa wabunge na Maseneta.

Waziri Mkuu Manuel Valls aliwashukuru maseneta kwa mtazamo wao. "Nimetaka kuwapongeza Maseneta kwa wajibu wao" amesema Waziri Mkuu.

Michel Mercier, mwandishi wa Kamati ya Sheria amepongeza mjadala huo. "Si muungano kati yetu, lakini ni umoja wa mapenzi ya nchi yetu," ameeleza.

Hali hii haikuzuia vyama vya mrengo wa kulia kudai uwajibikaji, hasa kwa kupitia kauli ya Dominique Estrosi Sassone, Seneta kutoka chama cha Republican katika eneo la Alpes-Maritimes. "Wakazi wa Nice bado wana hasira na wana haki. Hatuwezi kuendelea kutoa heshima kwa wahanga, kuendelea kusalia kimya kwa dakika kwa muda wa madakika na madakia, kuweka shada za maua, ameshauri Bii Estrosi Sassone. Kama hali ya hatari itaongezwa muda, ni lazima iwe kweli yenye muhimu na yenye ufanisi. "

Nakala ya maelewano iliandikwa wakati wa majadiliano makali usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi hii mwisho katika Jumatano na Alhamisi usiku.

Ombi la kuongezwa muda wa hali ya hatari litapitishwa Alhamisi hii wakati wa kusoma nakala hiyo, iliyofanyiwa marekebisho, katika Baraza la Bunge na Seneti.