UBELGIJI-USALAMA-UGAIDI

Ubelgiji: Siku kuu ya kitaifa chini ya ulinzi mkali

Ubelgiji inaadhimisha siku yake ya kitaifa Alhamisi hii, katika mazingira ya mashambulizi ya Machi 22 katika mji wa Brussels na mashambulizi ya mjini Nice tarehe 14 Julai. Ubelgiji bado iko chini ya tahadhari ya kigaidi, kwenye kiwango cha 3 kwa jumla ya 4.

Askari wa Ubelgiji wakipiga doria katika kituo cha biashara cha City 2, Brussels, Juni 15.
Askari wa Ubelgiji wakipiga doria katika kituo cha biashara cha City 2, Brussels, Juni 15. REUTERS/Francois Lenoir/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Hatua za usalama za ziadazimechukuliwa baada ya mashambulizi yaliyoikumba Ufaransa. Lakini gwaride, burudani na nsherehe mbalimbali zitafanyika.

Katika mji mkuu wa Ubelgiji, askari polisi na wanajeshi wamewkwa katika hali ya tahadhari. Hasa tangu hii Jumatano, Julai 20, mtu na mtoto wake walikamatwa katikati mwa mji, baada ya operesheni dhidi ya ugaidi, ambayo ilidumu kwa masaa yasiyopungua matano. Watu wliondolewa katika kituo cha biashara, eneo la hatari likazingirwa, maafisa wa kutegua mabomu walikua tayari wameshafika eneo hilo. Lakini mtu aliyepatika katika eneo hilo ambaye alishukiwa kuwa gaidi ni kijana anayesomea masuala ya mionzi mjini Brussels.

Tahadhari ya uongo, lakini ni ishara halisi ya hali ya hofuinayozunguka siku hii ya Siku kuu ya kitaifa. Meya wa jiji la Brussels ameelezea wasiwasi wake. "Watu wetu katika maeneo mbalimbali wamechoka, na wakati fulani tutachukua hatua za kiusalama! " amesema Yvan Mayeur.

Ratiba yabadilishwa

Lakini ratiba ya burudani na sherehe mbalimbali zitafanyika kama ilivyopangwa Alhamisi hii Julai 21. Gwaride la wanajeshi na raia litafanyika mchana kabla ya chakula. Raia wataweza pia kuhudhuria katika sherehe ya urushwaji wa fataki.

Maelekezo yalitolewa: watazamaji watawasili eneo hilo bila mfuko na kuacha magari yao nje katikati mwa jiji. Haijajulikana iwapo watu watakuja kwa wingi katika mazingira ya sasa.