UFARANSA-UINGEREZA

Hollande na May waonyesha maslahi yao ya pamoja

Rais Hollande na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Julai 21, 2016.
Rais Hollande na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Julai 21, 2016. REUTERS/Philippe Wojazer

Suala la kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, sheria yake na kalenda yake viligubika mkutano mjini Paris kati ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, na Rais wa Ufaransa François Hollande, Alhamisi, Julai 21, lakini viongozi hao wawili wa Ulaya wamenyesha uhusiano mzuri unaozingatia maslahi ya pamoja.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutaja shambulizi la mjini Nice na tishio la kigaidi, Rais wa Ufaransa na Waziri Mkuu wa Uingereza walionyesha dhamira ya nchi hizo mbili katika masuala nyeti ya kimataifa.

"Ushirikiano katika suala la ujasusi na usalama kati ya nchi zetu mbili utaendelea kuwepo daima, hata baada ya Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya. kujiondoa ina maana kujiondoa, Tutapata mafanikio, sisi pamoja na na washirika wetu wa Ulaya. Tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha usalama wa raia wetu na kuhifadhi maadili yetu duniani kote, " Theresa May amehakikisha.

Rais François Hollande amerejelea suala la kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. "Katika suala hilo hilo la majadiliano, ni kweli kuna haja ya kuwepo kwa maslahi ya nchi zetu mbili na maslahi ya Ulaya. Kesho ni kweli, Uingereza hautakuwa katika Umoja wa Ulaya, lakini kama Theresa May amesema hayo, Uingereza bado itakuwa katika Ulaya. Hatima ya Ulaya itahusu daima Uingereza, kama jinsi Ulaya itajihusisha daima na yale yanayoweza kutekelezwa na Uingereza duniani kote, amekumbusha rais wa Ufaransa. Hivyobasi, ufunguzi wa majadiliano lazima yajikite katika maslahi yetu. "

Na Waziri Mkuu wa Uingereza amekumbusha: utekelezaji wa Ibara ya 50 ya Mkataba wa Lisbon kwa kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya hautafanyika kabla ya mwisho wa mwaka.