UFARANSA

Wafuasi wa Islamic State wamemuua kwa kumkata shingo Padri nchini Ufaransa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande akitembelea kanisa lililovamiwa na magaidi hao
Rais wa Ufaransa Francois Hollande akitembelea kanisa lililovamiwa na magaidi hao Reuters

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema washambulizi wawili waliovamia kanisa moja la Katoliki katika mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray Kaskazini mwa nchi hiyo na kumkata shingo Padri Jacques Hamel mwenye umri wa miaka 84, walikuwa ni wafuasi wa kundi la Islamic State. 

Matangazo ya kibiashara

Wavamizi hao waliiingia ndani ya kanisa hilo wakati Padri huyo alipokuwa anaongoza misa na kutekeleza mauaji hayo ya kinyama pamoja na mateka wawili.

Mauaji haya yanakuja wiki mbili tu, baada ya watu wengine zaidi ya 80 kuuawa katika mji wa Nice baada ya kugongwa na Lori wakati wa sikukuu ya uhuru.

Rais Hollande amelaani mauaji hayo na kusema shambulizi hili linaonesha kuwa Ufaransa inaendelea kukabiliwa changamoto za kiusalama.

Rais huyo alizuru kanisa hilo, na kusema kuwa wananchi wa Ufaransa wanaugana na kanisa hilo kuomboleza kifo cha Padri huyo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amelaani mauaji hayo.