UFARANSA-USALAMA

François Hollande akutana na wawakilishi wa dini za Ufaransa

Rais wa Ufaransa anakutana na wawakilishi wa dini mbalimbali nchini Ufanransa(CRC) ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa Waislam, Katoliki, Orthodox, Kiprotestanti, Mayahudi na Ubuddha. Rais Hollande anatazamia pia kuongoza kikao cha baraza la usalama la kitaifa kabla ya kikao cha baraza la mawaziri.

Rais François Hollande, wakati wa hotuba yake katika Ikulu ya Elysée baada ya shambulio la mjini Saint-Etienne-du-Rouvray, Julai 26, 2016
Rais François Hollande, wakati wa hotuba yake katika Ikulu ya Elysée baada ya shambulio la mjini Saint-Etienne-du-Rouvray, Julai 26, 2016 Elysée
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake Jumanne hii Rais François Hollande alisema washambulizi wawili waliovamia kanisa moja la Katoliki katika mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray Kaskazini mwa nchi hiyo na kumkata shingo Padri Jacques Hamel mwenye umri wa miaka 84, walikuwa ni wafuasi wa kundi la Islamic State.

Wavamizi hao waliiingia ndani ya kanisa hilo wakati Padri huyo alipokuwa anaongoza misa na kutekeleza mauaji hayo ya kinyama pamoja na mateka wawili.

Mauaji haya yanakuja wiki mbili tu, baada ya watu wengine zaidi ya 80 kuuawa katika mji wa Nice baada ya kugongwa na Lori wakati wa sikukuu ya uhuru.

Rais Hollande amelaani mauaji hayo na kusema shambulizi hili linaonesha kuwa Ufaransa inaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama.

Rais huyo alizuru kanisa hilo, na kusema kuwa wananchi wa Ufaransa wanaungana na kanisa hilo kuomboleza kifo cha Padri huyo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amelaani mauaji hayo.