UFARANSA

Viongozi wa dini nchini Ufaransa wataka maeneo ya kuabudu kulindwa

Afisa wa usalama katika mji wa  Saint-Etienne-du-Rouvray,  baada ya Padri kuuawa kanisa
Afisa wa usalama katika mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray, baada ya Padri kuuawa kanisa REUTERS/Pascal Rossignol

Viongozi wa dini nchini Ufaransa wanataka maeneo ya kuabudu kulindwa baada ya kuuawa kwa Padri wa Kanisa Katoliki hapo jana Kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imekuja baada ya mkutano wa viongozi wa dini ya Kikiristo, Kiislamu, Kiyahudi na kibudha na rais Francois Hollande.

Padri Jacques Hamel mwenye zaidi ya miaka 80 aliuawa kwa kukatwa shingo na wavamizi wa Islamic State wakati akiongoza misa kanisani.

Rais Hollande amekutana na Waziri wa usalama lakini pia kuongoza Baraza la Mawaziri kujadili tukio hili.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa mauaji haya yanaonesha wazi kuwa kuwa nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto za kiusalama.

Mauaji haya yamekuja wiki mbili tu baada ya mfuasi wa Islamic State akiendesha Lori kuwagonga na kuwauwa watu 84 katika mji wa Nice.