UFARANSA-USALAMA

Ufaransa: viongozi serikalini watoa heshima ya mwisho kwa Padri aliyeuawa

Kutoka kushoto kwenda kulia: Nicolas Sarkozy, Valéry Giscard d'Estaing, Claude Bartolone, Gérard Larcher, Manuel Valls et François Hollande katika kanisa la Notre-Dame mjini Paris, Jumatano Julai 27.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Nicolas Sarkozy, Valéry Giscard d'Estaing, Claude Bartolone, Gérard Larcher, Manuel Valls et François Hollande katika kanisa la Notre-Dame mjini Paris, Jumatano Julai 27. REUTERS/Benoit Tessier

Siku moja baada ya shambulio katika mji wa Saint-Etienne-du-Rouvray lililomuua Padri mmoja katika kanisa lake, Rais François Hollande na viongozi wakuu wa kisiasa walikusanyika Jumatano hii, Julai 27 kwa misa katika kanisa la Notre-Dame mjini Paris.

Matangazo ya kibiashara

Waumini walikua wamefurika katika kanisa hilo. Watu1500 walikusanyika katika kanisa la Notre-Dame mjini Paris kwa kutoa heshima ya mwisho kwa Padri aliyeuawa katika shambulio mjini Saint-Etienne-du-Rouvray Jumanne Julai 26. "Bwana, tumekusanyika hapa katika amani ya upendo wako," alisema Kardinali André Vingt-Trois, askofu mkuu wa mjini Paris.

Kardinali alisema. "Matumaini kwa kutokabiliwa na chuki, njama na tuhuma," alisema. Hotuba hii ya Askofu Mkuu mjini Ufaransa. Katika misa hiyo walihudhuria Nicolas Sarkozy, Valéry Giscard d'Estaing, Claude Bartolone, Gérard Larcher, Manuel Valls na François Hollande

Itafahamika kwamba viongozi wa dini nchini Ufaransa walikutana Jumatano asubuhi na rais Hollande na kusema kuwa wanataka maeneo ya kuabudu kulindwa baada ya kuuawa kwa Padri wa Kanisa Katoliki Jumanne wiki hii Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kauli hiyo ilikuja baada ya mkutano wa viongozi wa dini ya Kikiristo, Kiislamu, Kiyahudi na kibudha na rais Francois Hollande.

Padri Jacques Hamel mwenye zaidi ya miaka 80 aliuawa kwa kukatwa shingo na magaidi wakati akiongoza misa kanisani.

Rais Hollande amekutana na Waziri wa usalama lakini pia kuongoza Baraza la Mawaziri kujadili tukio hili.

Kiongozi huyo alisisitiza kuwa mauaji haya yanaonesha wazi kuwa kuwa nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto za kiusalama.