ITALIA-TETEMEKO LA ARDHI

Zoezi la uokoaji laendelea Italia

Waokoaji wakiendelea na zoezi la kuwaokoa watu waliofukiwa chini ya vifusi vya majengo katika mji wa Amatrice (Italia), Agosti 24.
Waokoaji wakiendelea na zoezi la kuwaokoa watu waliofukiwa chini ya vifusi vya majengo katika mji wa Amatrice (Italia), Agosti 24. REUTERS/Stefano Rellandini

Maelfu ya waokoaji wamekuwa wakiendelea kuwatafuta manusura wa tetemeko la ardhi lilitokea nchini Italia Jumatano wiki hii na kusababisha zaidi ya watu 160 kufariki na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa idadi kubwa ya watu bado hawajapatikana na huenda wamezikwa katika vifusi vya majengo yaliyoanguka.

Serikali inasema waoakoaji zaidi ya 4000 wanaendelea kuwatafuta manusura wakitumia vifaa mbalimbali wakiwa na matumiani ya kuwapata baadhi yao wakiwa hai.

Wizara afya inasema idadi kubwa ya watu ambao wamepoteza maisha ni watoto na kuna uwezekano mkubwa sana idadi hiyo ikaongezeka.

Mtoto wa miezi 18 aliokolewa akiwa mzima katika vifusi vya majengo na anaendelea kupewa matibabu hopsitalini kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Italia.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.2 kwenye kipimo cha Richter lilitokea Jumatano wiki hii Kaskazini Mashariki mwa mji wa Rome.