UINGEREZA-UGADI-IS

Mhubiri wa kiislamu Choudary ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela

Anjem Choudary, London tarehe 31 Oktoba 2009.
Anjem Choudary, London tarehe 31 Oktoba 2009. REUTERS/Tal Cohen

Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali wa kidini Anjem Choudary, alihukumiwa Jumanne miaka mitano na nusu gerezani na mahakama ya London kwa kosa la kutoa wito wa kuunga mkono wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS).

Matangazo ya kibiashara

Kelele za Allah Akbar ( "Mungu ni Mkubwa"), zilizotolewa na wafuasi wake hamsini zimesikika katika ukumbi wa mahakama wakati uamuzi huo ulipokua ukitsomwa. Anjem Choudray, mwenye asili ya Pakistan ambaye ni mwanasheria, ni Mubiri wa kihistoria katika jamii Jamii ya Waislamu nchini Uingereza. Mhubiri huyu mwenye umri wa miaka 49alitoa wito wa kuunga mkono kundi la Islamic State katika mfululizo wa video zilizorushwa hewani katika mtandao wa You Tube. Katika mahubiri yake,alikula kiapo kushirikiana na kundi la Islamic State na mara kwa mara alikua akiimba nyimbo zinazomsifu kiongozi wake Abu Bakr al-Baghdadi.

Tangu miaka ya 1990, alionekana mwanaharakati mkubwa katika masuala ya dini alipokua akiandamana mbelea ya Misikiti ofisi za balozi mbalimbali na vituo vya polisi nchini Uingereza. Alijukina sana na viongozi pamoja vyombo vya habari kutokana na maandamano hayo. Lengo lake kuu, amekua akisema Anjem Choudary, ilikua kupandisha bendera ya Kiislamu kwenye 10, Downing Street, makazi ya waziri mkuu.

Choudary ni mmoja wa vigogo wakuu wa kundi la Waislamu wenye msimamo mkali wa kidini wanaoendesha harakati zao nchini Uingereza. Aliwahi kuongoza shirika la Kiislamu la Al-Muhajiroun, ambalo pia linajulikana kama "Islam4UK" katikati ya miaka ya 2000.