EU-ULAYA

Mkutano wa kilele bila Uingereza kwa kutoa msukumo mpya kwa EU

Mkutano wa Bratislavani wa kwanza tangu Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Mkutano wa Bratislavani wa kwanza tangu Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. REUTERS/Yves Herman

Marais na viongozi wa serikali kutoka nchi ishirini na saba za Umoja wa Ulaya wanakutana Ijumaa hii asubuhi Septemba 16 katika mji wa Bratislava, nchini Slovakia, ambayo ni mwenyekiti wa umoja huo wakati huu.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu, bila Uingereza, unaaminika kuwa ni hatua ya kwanza katika ujenzi wa Umoja wa Ulaya baada nchi hii kujiondoa. Lengo ni kutoa msukumo mpya kwa Ulaya ambayo inakabiliwa na matatizo mengi, lakini kazi ni ngumu.

"Bratislava ni mwanzo mchakato mrefu ambao utachukua muda kwa mageuzi ya Umoja wa Ulaya," kwa mujibu wa mwenyeji wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fixo.

Kikao cha kwanza kitagubikwa na majadiliano ya kisiasa juu ya hali ya Ulaya ambapo itakua ni fursa ya kukabiliana na masuala nyeti. Suala la mgogoro wa wahamiaji halitowekwa kando. Kati ya Italia na Ugiriki ambao wanaomba ushirikiano zaidi na nchi za Ulaya ya Kati ambao wanasita kuwapokea wahamiaji, tofauti ni nyingi na huenda kukaonekana mvutano katika mijadala itakayoendeshwa.

Ijumaa hii alasiri kutapewa nafasi kwa ufafanuzi wa vipaumbele na vitendo vya pamoja, ikiwa ni pamoja na usalama wa ndani na nje wa Umoja wa Ulaya, suala linalowatia wasiwasi viongozi wa Ulaya. Lakini mada nyeti, iliyopendekezwa na Ufaransa pamoja na Ujerumani itakuwa ile ya ulinzi wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na uanzilishwaji wa makundi ya kivita barani Ulaya, ufadhili wa shughuli za nje, kuanzishwa uongozi wa jeshi la Ulaya.

François Hollande na Merkel wanatakakuondoka katika mji wa Bratislava viongozi waote wa Ulaya wakiwa na mtazamo mmoja, ajenda iliyo wazi, lakini katika uwezekano wa kupambana na ugaidi, mgogoro wa wahamiaji.

Katika hotuba yake juu ya hali ya Umoja wa Ulaya, aliyoitoa Jumatano mbele yaBunge la Ulaya mjini Strasbourg, Jean-Claude Juncker alitoa wito kwa viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja huo watakaohudhuria mkutano wa viongozi wa Ulaya katika mji wa Bratislava kutafakari juu ya sababu za Umoja wa Ulaya. Katika mazingira ya "kuwepo kwake mgogoro" kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Ulaya, matarajio ya wabunge wa Ulaya ni makubwa.

Bendera za Umoja wa Ulaya na Slovakia, kabla ya mkutano wa Umoja wa Ulaya mjini Bratislava, Septemba 15, 2016.
Bendera za Umoja wa Ulaya na Slovakia, kabla ya mkutano wa Umoja wa Ulaya mjini Bratislava, Septemba 15, 2016. REUTERS/Yves Herman