HUNGARY-WAKIMBIZI

Sera ya Waziri Mkuu wa Hungary kutosahihishwa

Wananchi wakivaa nguo za kijadi wakati wa kura ya maoni dhidi ya wahamiaji katika mji wa Veresegyház, Jumapili hii, Oktoba 2, 2016.
Wananchi wakivaa nguo za kijadi wakati wa kura ya maoni dhidi ya wahamiaji katika mji wa Veresegyház, Jumapili hii, Oktoba 2, 2016. REUTERS/Bernadett Szabo

Wananchi wa Hungary walitakiwa kupiga kura kwa kura ya maoni Jumapili hii, Oktoba 2 kwa kuunga au kupinga dhidi ya kuhamishwa kwa wakimbizi nchini humo. Hoja hii ilianzishwa na Waziri Mkuu ambaye alitaka kuidhinisha sera yake ya kupambana dhidi ya wahamiaji.

Matangazo ya kibiashara

Karibu wa wapiga kura wote walipiga kura ya "Hapana" kwa sera ya Ulaya ya kugawana wahamiaji, lakini ushiriki katika kura hii ya maoni ulifikia katika kiwango cha 40%. Hata hivyo ilikua inahitajika 50% ya kura ili sera hiyo ya Waziri Mkuu iweze kupitishwa. Umoja wa Ulaya "hauwezi kulazimisha nia yake kwa Hungary," amejibu, Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban.

Licha ya kampeni ya vitisho kwa wananchi wa Hungary, chama cha Waziri Mkuu Viktor Orban kimeshindwa kuhamasisha wapiga kura wa kutosha. Kwa mujibu wa takwimu rasmi ushiriki ulikua katika kiwango cha chini ya 45% na kura zote zilizopigwa zilifikia 40%, jambo ambalo linapelekea sera ya Waziri Mkuu kufutiliwa mbali.

Mashirika mengi yasio ya kiserikali yalikua yalitoa wito wa kutosahihisha sera ya Waziri Mkuu Viktor Orban.Upinzani ulikua uliwatolea wafuasi wake kususia kura hiyo ya maoni. Wafuasi wa vyama kadhaa vya upinzani wilionekana wakifura hiyo ushindi huo dhidi ya sera ya Waziri Mkuu, Jumapili hii usiku walipokua walikusanyika katika baa moja ya mjini Budapest.

Kwa mujibu wa Zsuzsanna Szelenyi, mbunge kutoka chama kidogo cha mrengo wa kushoto cha Ensemblen, matokeo haya ni habari njema. "Serikali ya Hungary ilikua ikifanya kampeni kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Ilikuwa ni kampeni ya chuki, kwa hiyo tunafurahia sana kwa matokeo haya. "

Upinzani unadai Orban ajiuzulu

Huu ni ushindi, amesema kiongozi wa chama cha MHM. Kwa jambo hili, "taifa la Hungary limeweza kuokoa heshima yake ya uzalendo". Amemtaka Waziri Mkuu kujiuzulu.