UBELGIJI-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Askari polisi wawili wajeruhiwa kwa kisu Brussels

Eneo lililotengwa kwa usalama katika eneo la shambulio la askari polisi wawili, Oktoba 5, 2016 mjini Brussels.
Eneo lililotengwa kwa usalama katika eneo la shambulio la askari polisi wawili, Oktoba 5, 2016 mjini Brussels. AFP/Dirk Waem

Askari polisi wawili wameshambuliwa na kujeruhiwa kwa kisu mjini Brussels Jumatano hii na mwanajeshi wa zamani wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 43, ambaye inaonekana alifanya hivyo kwa sababu za 'ugaidi'. Mwanajeshi huyo wa zamani alikamatwa, kwa mujibu wa taarifa za kwanza za uchunguzi.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi wawili, mwanamume na mwanamke, walishambuliwa saa sita mchana na mtu aliyekuwa amejihami kwa kisu kwenye barabara kuu ya wilaya ya Schaerbeek mjini Brussels, Ofisi ya mashitaka imebaini. Askari polisi mmoja amejeruhiwa 'tumboni' na mwengine 'shingoni', lakini wanaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Schaerbeek, Bernard Clerfayt, mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo anasema alimuona mtu mmoja akimchoma kwa kisu mgongoni askari polisi mmoja ambaye alikua akitokea katika hospitali jirani na mwenzake.

'Wamejeruhiwa' lakini wanaweza kutoka hospitali usiku wa leo, amesema Bw Clerfayt kwenye kituo cha redio binafsi cha RTL-TVI.

"Nilionamshambuliaji akimpiga askari polisi hadi anagaaga chini. Alipata ngumi na mateke. Askari polisi alikimbia kichakani lakini alifuatwa na kuendelea kupigwa. Baadaye mwanamke aliyekua akiambatana na askari polisi hyo alipigwa, huku akilia na kutokwa na damu. muda mchache baadaye polisi iliwasili katika eneo la tukio na kuweza kumpiga mshambuliaji huyo risasi mguuni, " shahidi amesema kwenye runinga ya taifa ya RTBF.

"Matokeo ya utafiti wa awali unaonyesha kwamba kuna uwezekano kuwa kitendo ni shambulizi la kigaidii," Ofisi ya mashitaka imesema, huku ikimtambua mtuhumiwa kama 'Hicham D., ambaye alizaliwa Aprili 26, 1973, nchini Ubelgiji'.