UJERUMANI-UGAIDI

Ujerumani: mshukiwa wa shambulio la ugaidi ajinyonga akiwa gerezani

Mkimbizi kutoka Syria anayetuhumiwa kutaka kutekeleza shambulizi nchini Ujerumani kwa niaba ya kundi la Islamic State (IS) alijiua gerezani Jumatano hii, siku mbili baada ya kukamatwa kwake, na hivyo kuzusha hali ya sintofahamu kuhusu mazingira yake ya kuzuiliwa.

Hendrik Schmidt / dpa / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jaber al-Bakr alijiua akiwa katika chumba chake katika gereza la Leipzig," serikali ya mkoa wa Saxe, mashariki mwa Ujerumani, imesema katika taarifa yake, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Mkutano na waandishi wa habari utafanyika Alhamisi hii kuhusu tukio hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild na shirika la habari la DPA, mtuhumiwa alikutwa amejinyonga katika chumba chake ambapo alikua akizuiliwa. Aliwekwa jela tangu Jumatatu wiki hii katika mji Saxe.

"Ninasikitishwa na siamini kwa kile kilichotokea," mwanasheria wake, Alexander Hübner ameliambia gazeti la Focus, huku akitaja kesi hiyo kuwa ni 'kashfa kwa mahakama.' Hatari ya kujiua kwa mteja wake ilikua inajulikana kwa viongozi wa jela, alisema, akibainisha kwamba alikuwa amegoma kula tangu kuzuiliwa kwake na alijaribu kujiua kwa kumia umeme bila mafaanikio. Kwa mujibu wa wa gazeti la Bild, chumba chake kilikua kikikaguliwa mara moja kwa saa.

Jaber al-Bakr alikamatwa baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kwa kushukiwa kupanga shambulizi la uwanja wa ndege wa Berlin.

Polisi wanasema walikuta gramu 1.5 ya bomu ndani ya ghorofa yake katika mji wa Chemnitz. Vyombo vya usalama nchini Ujerumani wanasema walipokea taarifa wiki iliyopita kuwa mshukiwa huyo alikua akitumia mtandao kupata maelekezo ya kutengeneza mabomu.