UINGEREZA-CALAIS-WAHAMIAJI

Vipimo vya meno kwa watoto vyazua utata Uingereza

Wahamiaji 9,000 wapewa hifadhi katika kambi ya Calais
Wahamiaji 9,000 wapewa hifadhi katika kambi ya Calais AFP

Madaktari wa meno nchini Uingereza wamesema hawakubaliani na vipimo vya meno kwa watoto wahamiaji kutoka katika mji wa Calais waliowasili nchini Uingereza hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Pendekezo la kufanya vipimo vya meno kwa watoto hawa limetolewa na chama kimoja nchini Uingereza kinachoshiriki katika serikali ya mseto.

Pendekezo hili limezua hali ya utata nchini Uingereza ambapo watoto wasio na wazazi wamejiunga na familia zao, kutoka kambi ya Calais.

Vipimo vya meno vinaonyesha umri halisi wa mtu, na kujua kama mtu huyo bado ni mdogo au la.

David Davies, Mbunge wa chama cha Monmouth, amesema vipimo hivi vinaweza kuwahakikishia wananchi wa Uingereza kuhusu umri wa wahamiaji.

Lakini British Dental Association, chama cha madaktari wa meno nchini Uingereza, kimesema kwamba vipimo hivi ni kinyume na maadili ya kimatibabu.