UBELGIJI-CANADA-USHIRIKIANO

CETA: EU yatoa kauli ya mwisho kwa Ubelgiji

Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, akisubiri Jumatatu hii Oktoba 24 kuona msimamo wa Ubelgiji kuhusu kusaini mkataba wa biashara huria na Canada.
Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, akisubiri Jumatatu hii Oktoba 24 kuona msimamo wa Ubelgiji kuhusu kusaini mkataba wa biashara huria na Canada. REUTERS/Eric Vidal

Jumapili hii Oktoba 23, Umoja wa Ulaya umeionya Ubelgiji hadi Jumatatu jioni kuwa imetoa msimamo wake wa 'Ndio' au 'Hapana' kama inaweza kusaini mkataba wa biashara huria na Canada (CETA) , onyo ambalo limefutiliwa mbali na serikali ya Wallonia ambayo inazuia mkataba huo.

Matangazo ya kibiashara

Lakini Waziri Mkuu wa Wallonia, Paul Magnette, ambaye upinzani kwa CETA unazuia kupitishwa kwake na Umoja wa Ulaya, anaona kuwa onyo hilo "si sambamba na mchakato wa kidemokrasia," msemaji wake ameliambia shirika la habari la AFP.

Bw Magnette "amekataa kukubali muda wa kulazimishwa," amesema msemaji wake.

Umoja wa Ulaya umeitaka ubelgiji hadi Jumatatu hii jioni imwe imekwisha toa idhini yake, vinginevyo mkutano na zoezi la kusaoni vilivyopangwa kufanyika Alhamisi wiki hii mjini Brussels, akiwepo Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau vitafutwa.

Ubelgiji ni moja ya nchi 28 za Umoja wa Ulaya ambayo inakabiliwa na hali ya sintofahamu ya kusaini mkataba wa CETA, mkataba unaohusu zaidi ya milioni 500 kutoka Umoja wa Ulaya, kutokana na kuzuia na serikali ya Wallonia, jimbo lenye wakazi milioni 3.6 wanaozungumza Kifaransa.

Kabla ya 'Jumatatu usiku'

'Jumatatu hii jioni, Rais wa Baraza la Ulaya --linalowakilisha nchi 28 za umoja wa Ulaya, Donald Tusk atakua na mazungumzo kwa simu ' na Justin Trudeau, "kuamua kama mkutano utafanyika, " chanzo Umoja wa Ulaya kimelieleza shirika la habari la AFP.