UBELGIJI-HAKI

Mfalme wa zamani wa Ubelgiji akabiliwa na kesi ya kumtambua mwanawe

Mfalme wa zamani wa Ubelgiji akiwa na Malkia Paola wakati wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 80 ya kuzaliwa kwake, ilikua mwaka 2014.
Mfalme wa zamani wa Ubelgiji akiwa na Malkia Paola wakati wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 80 ya kuzaliwa kwake, ilikua mwaka 2014. REUTERS / Laurent Dubrule

Mfalme wa zamani wa Ubelgiji Albert II ametakiwa kuripoti mahakamani mwezi Februari mwakanikatika kesi ya msanii wa Ubelgiji ambaye anataka kutambuliwa na mfalme huyo wa zamani kama binti yake, alisema Jumanne hii mwanasheria wa mlalamikaji.

Matangazo ya kibiashara

Delphine Boel, mwenye umri wa miaka 48, kwa zaidi ya miaka 10 anatafuta kutambua kwamba yeye ni binti wa mfalme wa zamani wa Ubelgiji. Albert II hajawahi kueleza hadharani juu ya suala hilo.

"Mahakama imeamuru kwamba watu wanaohusika na kesi hii wanatakiwa kufika mahakamani", mwanasheria Alain De Jonge ameliambia shirika la utangazaji la Reuters, huku akiongeza kuwa mfalme anapaswa kufika mahakamani tarehe 21 Februari mwaka 2017.

Albert II leo ana umri wa miaka 82. Alijiuzulu mwaka 2013 na kumuachia nafasi mwanawe Philippe.