UFARANSA-USALAMA

Polisi wa Ufaransa waomba kuzungumza moja kwa moja na wabunge

Askari polisi waandamana nje ya jengo la Bunge mjini Paris Oktoba 26, 2016.
Askari polisi waandamana nje ya jengo la Bunge mjini Paris Oktoba 26, 2016. REUTERS/Charles Platiau

Polisi wa Ufaransa wamepandwa na hasiri. Kwa zaidi ya wiki, wamekua wakikusanyika kila jioni wakidai mazingira mazuri ya kazi, uwezo wa kutoshai, na kutambuliwa vema kwa kazi wanayoifanya.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii Oktoba 26 wakati wa mchana, saa 8:00, maafisa 500 wa polisi walikusanyika nje ya jengo la Bunge mjini Paris, ili kuweka shinikizo kwa Rais Francois Hollande, ambaye amekutana jioni ya Jumatano hii na vyama vyao.

Kwenye eneo la Concorde, polisi hao walikusanyika wakiwa na mabango yaliyoandikwa "maisha yetuyanachangia" au "polisi yangu, vita vyangu." Hata hivyo, hakuna bendera ya chama cha olisi iliyopandishwa kwenye eneo hilo. Na kwa mujibu wa mlinzi wa amani mjini Paris, si ajabu. "Leo hii tupo hapa bila vyama vya wafanyakazi. Tunakuja ili tuweze kusikilizwa. Inabidi kundi hili, ambalo ni chanzo cha hali hii, liweze kusikilizwa, na wala si wawakilishi ambao hatuwataki, amesema mlinzi huyo wa amani wa mji wa Paris.

"Hakuna tena mawasiliano na vyama vya wafanyakazi, ni lazima kutafuta njia nyingine ya kusikilizwa. Wakati tutakua bado hatujasikilizwa, tutaendelea na harakati zetu. Uchovu? Ni kawaida, ni muda mrefu sasa uchovu huo tunao, tutaendelea, "ameongeza. Wengi wanalaumu vyama vya wafanyakazi kutokua na mawasiliano na wanachama wao na kutojali. Baadhi ya maafisa wanaona kuwa yameingizwa kisiasa, na yako mbali kwa majukumu ya kila siku ya polisi.