UINGEREZA-EU

Serikali ya Uingereza mbioni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akipania kuanzisha mchakato wa kujionda katika Umoja wa Ulaya..
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akipania kuanzisha mchakato wa kujionda katika Umoja wa Ulaya.. REUTERS/Dylan Martinez

Serikali ya Uingereza imesema itakata rufaa baada ya Mahakama kuu jijini London kuamua kuwa, mchakato wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya hauwezi kuanza hadi pale Bunge litakapojadili suala hilo.

Matangazo ya kibiashara

Majaji Watatu wa Mahakama hiyo waliamua kuwa Waziri Mkuu Theresia May hana mamlaka ya kuanzisha mchakato huo wa kuimbia Umoja wa ulaya kuwa inajiondoa rasmi.

Katika ya mwaka huu raia wa Uingereza walipiga kura ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na Waziri Mkuu May amekuwa akiahidi kuanza mchakato wa kujiondoa kufikia mwezi Machi mwakani.

Mahakama kuu ya jijini London, Uingereza ilitoa uamuzi ikisema kuwa, ni Bunge ndilo linalopaswa kuidhinisha mpango wa nchi hiyo kujiondoa kwenye umoja wa Ulayana na sio serikali, uamuzi ambao sasa huenda ukachelewesha zoezi la nchi hiyo kuanza mchakato wa kujitoa.

Uamuzi huu umekuja ikiwa ni miezi michache tu imepita, toka waziri mkuu Theresa May atangaze kuwa nchi yake imeanza mchakato wa kutengua ibara ya 50 ya mkataba wa Lisbon, mchakato utakaoshuhudia nchi hiyo ikijiondoa rasmi kwenye umoja huo ndani ya muda wa miaka miwili.