UFARANSA-USALAMA

Ufaransa yaadhimisha mwaka mmoja tangu mashambulizi ya kigaidi jijini Paris

Raia nchini Ufaransa waadhimisha mwaka mmoja tangu mashambulizi ya kigaidi Paris
Raia nchini Ufaransa waadhimisha mwaka mmoja tangu mashambulizi ya kigaidi Paris REUTERS/Benoit Tessier

Raisi wa Ufaransa hii leo ameongoza maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea mashambulizi ya kigaidi jijini Paris yaliyoua takribani watu 130.

Matangazo ya kibiashara

Raisi Hollande na meya wa jiji la Paris Anne Hidalgo walifunua sanamu nje ya uwanja wa taifa wa Stade de France, ambako washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga walilipua vilipuzi vyao wakati wa mechi ya kimataifa ya soka na kuua mtu mmoja na kuendelea na mfululizo wa mashambulizi.

Maadhimisho hayo yalipangwa pia katika jumba la Bataclan, ambako takribani watu 90 waliuawa wakiwa tamashani baada ya washambuliaji watatu kuvamia eneo hilo.

Hapo jana Usiku nyota wa muziki wa Rock maarufu kwa jina la Sting alizindua tamasha la kufungua tena jumba la michezo ya kuigiza la Bataclan ambako pia wanajihadi waliua watu 90.

Mwanamuziki huyo baada ya kuwataka mashabiki kutulia kimya kwa dakika moja kutoa heshima kwa watu waliopoteza maisha katika shambulizi hilo alisema hawatasahaulika.

Uchunguzi wa mashambulizi yaliosababisha vifo vya watu wengi nchini Ufaransa ulipelekea katika siku mbili kubaini watatu kati ya watu saba waliojitoa mhanga, wakati ambapo wito kwa mashahidi ulitolea Novemba 15 mwaka jana ili kumpata ndugu wa mmoja wao,anayechukuliwa kama "mtu hatari.