UFARANSA

Ufaransa: Aliyekuwa waziri wa Hollande, Emmanuel Macron atangaza kuwania urais

Waziri wa zamani wa uchumi nchini Ufaransa, Emmanuel Macron, ameapa kufanya "mapinduzi ya demokrasia" wakati huu akitangaza rasmi kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Emmanuel Macron, kiongozi wa chama kipya cha "En Marche", ametangaza kuwania urais, 5 Novemba 2016.
Emmanuel Macron, kiongozi wa chama kipya cha "En Marche", ametangaza kuwania urais, 5 Novemba 2016. REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Mfumo wa kisiasa ulishaoza, alisema "nataka kuruhusu nguvu ya wanaojiweza wakati nikiwalinda wasiojiweza".

Licha ya kuwa alihudumu kwenye utawala wa rais Francois Hollande, kiongozi huyu mwenye mrengo wa kati, atawania kiti cha urais kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Uamuzi wake wa kuwania urais, tayari umetikisa kambi za vyama vyote vya mrengo wa kushoto na ule wa kulia, akitarajia kuwa mbadala wa vyama vyote viwili.

Chama hiki chenye msimamo wa kati, kitaanza kuchagua wagombea wake kwa mfumo mpya kama ule uliotumiwa na wamarekani kwa kuanzia kwenye majimbo.

Aliyekuwa kinara kwenye mbi hizo Alain Juppe, amemtuhumu Macron kwa kumsaliti rais Hollande, na kuongeza kuwa hakuna tofauti na "mtu anaemchoma mtu kisu kwa nyuma."

Wakati mmoja akitajwa kuwa mtu wa karibu wa rais Hollande, Macron alijiondoa kwenye kwenye serikali inayoongozwa na chama cha Kisocialist mwezi August mwaka huu, baada ya kutokea mvutano ndani ya chama hicho kuhusu nafasi za kisiasa.

Mpaka sasa rais Hollande mwenyewe bado hajatanagaza ikiwa atawania tena kiti hicho kwenye uchaguzi wa mwezi April mwakani, na anatarajiwa kufanya maamuzi ndani ya wiki chache zijazo.

Hollande ndiye mgombea ambaye mpaka sasa ana umaarufu mdogo zaidi kuwahi kutokea.