UFARANSA-UTAFITI

Wanaanga watatu walazimika kusitisha utafiti wao kuhusu sayari mpya

Sayari ya Jupiter,iliyopigwa picha mwaka 1979.
Sayari ya Jupiter,iliyopigwa picha mwaka 1979. (Photo by: Universal History Archive/UIG via Getty Images)

Kikosi cha wanaanga watatu waliopanga kuendelea na utafiti wao kugundua sayari Mpya kwa muda wa miezi sita wamelazimika kusitisha utafiti wao huo leo Ijumaa, baada ya mtambo waliotumia Soyuz kulipuka.

Matangazo ya kibiashara

Wanaanga hao ni pamoja na Mfaransa Thomas Pesquet, lakini pia Oleg Novitsky raia wa Urusi naye Peggy Whitson wa idara ya mambo ya anga ya Marekani NASA.

Itakumbukwa mwezi Juni mwaka huu Chombo cha utafiti cha idara ya mambo ya anga ya Marekani NASA kinachojulikana kama Juno kimetuma picha yake ya kwanza ya sayari ya Jupiter toka kilipowasili katika sayari hiyo.

Idara hiyo ya Marekani imetoa picha inayoionyesha sayari ya Jupiter ikiwa imezungukwa na miezi yake minne mikubwa.