UFARANSA-UGAIDI

Ufaransa yawaachia huru watuhumiwa wawili wa ugaidi

Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls
Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls REUTERS/Jacky Naegelen

Mamlaka nchini Ufaransa, zimewaachia huru, watuhumiwa wawili kati ya saba, waliokamatwa mwishoni mwa juma lililopita na polisi, kufuatia operesheni iliyofanikisha kuzuia jaribio la ugaidi. 

Matangazo ya kibiashara

Polisi wa Ufaransa, Jumapili usiku waliendesha msako maalumu mashariki mwa mji wa Strasbourg na Kusini mwa mji wa Marseille, baada ya upelelezi walioufanya kwa saa zaidi ya 8.

Polisi iliwakamata watu saba wanaotuhumiwa kupanga njama za kutekeleza ugaidi kutoka Ufaransa, Morocco na Afghanistan, operesheni ambayo waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneueve alisema mkakati uliokuwa umepangwa muda mrefu.

Watuhumiwa wawili kati ya saba waliokamatwa Marseille, wameachiwa usiku wa kuamkia Jumatano, Novemba 23.

Watu hawa walidaiwa kuwa huenda walikuwa wanawapatia hifadhi watuhumiwa wawili wa ugaidi kutoka Morocco, ambao wenyewe bado wanaendelea kushikiliwa.

Nchi ya Ufaransa bado imeendelea kusalia chini ya hali ya hatari, ambayo inawapa mamlaka polisi kutumia nguvu kuendesha msako dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi, mwaka mmoja baada ya shambulio la Paris.

Nchi ya Ufaransa mpaka sasa imeshuhudia mashambulizi matatu makubwa toka mwezi january mwaka 2015, wakati watu wenye silaha waliposhambulia ofisi za gazeti la Charlie Hebdo na duka la kiyahudi na mwezi Novemba mwaka jana kutekeleza shambulio baya zaidi jijini Paris.

Mwezi Julai mwaka huu pia, mtuhumiwa wa ugaidi rais wa Tunisia, aliwaua watu 86, baada ya kuendesha lori la mizigo kwenye umati wa raia mjini Nice.