EU-BUNGE

Martin Schulz afuta nia yake ya kuwania muhula mpya katika Bunge la EU

Rais wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz, raia wa Ujerumani, amesema Alhamisi hii kwamba anafuta nia yake ya kuwania, mwezi Januari, muhula wa tatu katika uongozi wa taasisi hiyo ili kujikita katika kuandaa kuwania katika uchaguzi wa bunge nchini Ujrumani utakaofanyika mwezi Septemba 2017.

Martin Schulz, Rais wa Bunge la Ulaya, Novemba 24, 2016 mjini Brussels.
Martin Schulz, Rais wa Bunge la Ulaya, Novemba 24, 2016 mjini Brussels. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

"Sintokuwa mgombea wa awamu ya tatu kama rais wa Bunge la Ulaya," amesema raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 60, katika ujumbe uliosoma kutoka Brussels na kurushwa kwenye mtandao wa ndani ya Bunge.

"Mwaka ujao, nitawania katika uchaguzi wa bunge (Bundestag) kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya wagombea kutoka chama cha SPD (Social Democratic Party) Kaskazini- mwa Westfalia" Bw. Schulz ameongeza.

Martin Schulz, ambaye mara kwa mara anatajwa kama mgombea wa chama SPD katika uongozi wa nchi ya Ujerumani dhidi ya Angela Markel wa chama cha CDU, ambaye alitangaza Jumapili kuwa atakuwa mgombea kwa muhula wa nne.

Waziri wa sasa wa Ujerumani mwenye dhamana ya Mambo ya Nje, Frank-Walter Steinmeier, mwezi Februari atakuwa rais wa Ujerumani, na kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani, rais wa Bunge la Ulaya anapewa nafasi kubwa ya kmrithi kwenye wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani.