Hati ya kutafutwa ya EU kwa mtuhumiwa wa shambulizi la mjini Berlin yatolewa
Imechapishwa:
Serikali ya Ujerumani imeongeza kasi kwa kumsaka mtuhumiwa wa shambulizi la mjini Berlin, aliyekua akiendesha lori usiku wa Jumatatu katika mji huo, wakati alipoingia katika umati wa watu katika soko la bidhaa vya krismasi, na kuua watu wasiopungua 12 na kuwajeruhi wengine 48.
Kundi la Islamic State lilidai kuwa askari wake ndio alihusika na kitendo hicho. Polisi ilimtambua mtuhumiwa kama raia wa Tunisia mwenye umri wa miaka 24, ambayeanatafutwa kwa udi na uvumba. Hati ya kutafutwa ya Umoja wa Ulaya ilitolewa usikuwa kuamkia Ahamisi hii.
Wachunguzi kutoka Ujerumani wlitambua haraka kwamba hawakuwa na ushahidi wa kutoshawa kuhusisha tukio hili kati ya mtuhumiwa wa kwanza aliyekamatwa baada ya shambulio hilo, ambaye ni raia kutoka Pakistan aliyekua akitafuta hifadhi ya ukimbizi, na shtuma dhidi yake. Mtuhumiwa huyo aliachiwa siku ya Jumanne na muhusika wa shambulio hilo bado hajapatikana.
Mtuhumiwa tayari ametambuliwa na serikali ya Ujerumani
Polisi ya Ujerumani imeongeza kasi ya kumsaka mtuhumiwa huyo, raia wa Tunisia, ambaye kibali chake cha uraia kilipatikana chini ya kiti cha dereva wa lori. Mtuhumiwa huyo anajulikana kwa jina la Anis Amri, raia wa Tunisia, mwenye umri wa miaka 24, ambaye urefu wake ni mita 1,78, huku akipima kilo 75. hati ya kutafutwa imetolewa na "kitita cha Euro 100 000 kimetolewa kwa yeyote yule atakayemkamata au kuficghua sehemu alipo," kitendo cha ugaidi katika Ofisi ya mashitaka nchini Ujerumani imesema katika taarifa yake.