UJERUMANI-SHAMBULIZI-USALAMA

Shambulizi la Berlin: alama za vidole za mtuhumiwa zapatikana katika lori

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere ametangaza Alhamisi hii kwamba alama za vidole vya mtuhumiwa, raia wa Tunisia, mwenye umri wa miaka 24, zimepatikana katika lori lililotumiwa katika shambulizi na kuua watu 12 katika soko la bidhaa vya Krismasi mjini Berlin.

Alama za vidole vya mtuhumiwa zimepatikana kwenye sehemu mbele ya lori iliyotumiwa katika shambulizi dhidi ya soko la bidhaa za Krismasi mjini Berlin.
Alama za vidole vya mtuhumiwa zimepatikana kwenye sehemu mbele ya lori iliyotumiwa katika shambulizi dhidi ya soko la bidhaa za Krismasi mjini Berlin. REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo Anis Amri akiendelea kukosekana, ushiriki wake katika shambulio la mjini Berlin hauna tena shaka. Alhamisi hii, Thomas de Maiziere ametangaza kuwa alama za vidole vya raia huyo kutoka Tunisia, mwenye umri wa miaka 24 zimepatikana kwenye sehemu ya mbele ya lori ambayo iliingizwa katika umati wa watu katika soko la bidhaa vya Krismas katika mji mkuu wa Ujrymani, na kusababisha vifo vya watu 12 na kuwajeruhi wengine wengi. "Leo hii tunaweza kutangaza kwamba kuna dalili ya ziada ambayo mtuhumiwa pengine ni kweli muhusika wa shambulizi, " amesema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani.

jina la Anis Amri lilionekana Jumatano Desemba 21 baada ya kibali cha cha kuishi Ujerumani kupatikana katika sehemu ya mbele ya lori. Hati ya kutafutwa ilitolewa, na kitita cha Euro 100,000 kimetengwa kwa mtu atakaye mkamata au kuonyesha aliko Anis Amri.

Anis Amri aliyewasili nchini Ujerumani mwaka 2015, alikua anajulikana na vyombo vya usalama. Alikua akitafutwa kwa uchunguzi kwa ajili ya maandalizi ya shambulizi na alikuwa chini ya uchunguzi kwa mwaka 2016. Uchunguzi hatimayeulifutiliwa mbali mwezi Septemba kwa kukosa ushahidi. Anis Amri pia alikuwa anaatuhumiwa wizi ili kugharamia ununuzi wa silaha za kivita. Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, alijaribu kuajiri washirika miezi kadhaa iliyopita.