UINGEREZA-ELIZABETH II

Malkia Elizabeth ashindwa kuhudhuria ibada ya Krismasi

Malkia wa Uingereza ameshindwa kuhudhuria ibada ya krismas kwa kuwa bado anaugua homa kali. Buckingham Palace imesema kuwa anaendelea kusalia nyumbani ili kumsaidia kupona lakini ikaongezea kuwa atahudhuria sherehe za krismas za familia.

Malkia wa Uingereza, Elizabeth II na Prince Philip, Jumatano, Mei 9, 2012, mjini London.
Malkia wa Uingereza, Elizabeth II na Prince Philip, Jumatano, Mei 9, 2012, mjini London. euters / Oli Scarff
Matangazo ya kibiashara

Ni nadra kwa malkia, mwenye umri wa miaka 90, kufuta safari kwa sababu za kiafya.

"Malkia hatahudhuria ibada ya Krismas katika kanisa la Sandringham leo asubuhi. Malkia anaendelea kupata nafuu kutokana na homa kali iliyompata, " Buckingham Palace ilitangaza mapema Jumapili hii asubuhi. Malkia Elizabeth II, ambaye aliadhimisha miaka yake 90 ya kuzaliwa mwezi Aprili, alibakia katika makazi yake ya Sandringham, mashariki mwa Uingereza, ambapo familia ya kifalme inaadhimisha kama kawaida sherehe za Mwaka Mpya. "Malkia atahudhuria sherehe za Krismasi za familia ya kifalme wakati wa mchana," ilisema taarifa ya Buckingham Palace.

Kutoka kilomita 300, katika mji wa Englefield, kusini mwa Uingereza, Prince George (miaka 3) na Princess Charlotte (mwaka 1), wajukuu wa Malkia, wao walihudhuria ibada yao ya kwanza ya Krismasi na wazazi wao, Prince William na Kate.

Mapema wiki hii, Malkia na mumewe Philip, mwenye umri wa miaka 95, walifuta safari yao katika mji wa Sandringham, kwa sababu ya homa hiyo.