Ufaransa: François Hollande atoa msamaha kwa Jacqueline Sauvage
Imechapishwa:
Rais wa Ufaransa François Hollande ametoa msamaha kamili kwa Jacqueline Suavage, mwanamke aliyehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumua mumewe aliyekua akimdhalilisha kwa kumpiga kila mara.
"Rais François Hollande amesema kuwa nafasi ya Bi Sauvage si tena gerezani, lakini karibu na familia yake," taarifa kutoka Elysee imeeleza. Jacqueline Sauvage, aliyehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela kwa mauaji ya mume wake, anaweza kuondoka gerezani mara moja, Ofisi ya rais imesema.
"Nimeamua kutoa msamaha kwa Jacqueline Sauvage ili kufuta hukumu yake. Msamaha huu unasitisha mara moja kifungo chake cha miaka 10 jela," amesema rais wa Ufaransa kwenye akaunti yake ya Twitter.
Mnamo mwezi Oktoba 2014, Jacqueline Sauvage alihukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani kwa mauaji ya mume wake aliyekua kimdhalilisha kwa kumpiga mara kwa mara.
Hukumu hii ilithibitishwa tarehe 4 Desemba 2015 na Mahakama ya Rufaa ya Blois.
Mapema mwaka 2016, rais wa Ufaransa alitoa nusu ya mshamaha kwa bii Sauvage, ambapo ulimpeleke aombe kuachiwa kwa masharti, lakini ombi hilo lilikataliwa na mahakama.